MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Kesho Taifa linaingia vitani kwenye soka kusaka heshima, na kujiweka kwenye ramani mpya ya ulimwengu wa michezo duniani kwa kufuzu Afcon.
Tunapokuwa kwenye nyakati kama hizi kitaifa ni vizuri tukawa kitu kimoja na kuelewana kwenye malengo ya kuhakikisha timu ya Taifa inashinda.
Nimeona lawama kwa kamati ya kuhamasisha kutumia wasanii mbalimbali kuhamasisha watanzania badala ya kutumika wachezaji wa zamani na waandishi wa habari za michezo wa zamani.
Sikatai umuhimu wa hao legends kuhamasisha lakini lazima tukubaliane tume target kundi gani. Ile press ya akina Manara na maudhui yote yalikuwa kuhamasisha wananchi kuujaza uwanja wa taifa ili kusaidia kuhamasisha timu.
Nimeshuhudia wachezaji wa zamani akiwemo akina Peter Tino wakiitwa kwenye kambi ya timu ya taifa kuongea na wachezaji na ushawishi na umuhimu wao mkubwa upo huko. Lakini swala la kutangaza na kuhamasisha wananchi kwa zama zetu hizi za mitandao lazima utatumia vijana wenye influence kwasasa.
Tuache kulalamika hadi kwenye nyakati ambazo tunapaswa kuwa kitu kimoja. Inasikitisha sana tunaacha kuhamasishana na kuanza kuandika makala ndefu za lawama kwa watu ambao wanafanya kwa nia njema.
Tuchukulie mfano mdogo, Haji Manara amefanikiwa kuinfluence wana Simba kuujaza uwanja wa Taifa na kuwa chachu ya ushindi kwa mechi za hapa nyumbani. Vipi akiungana na stars wengine kuhamasisha wananchi, hamasa itakuwa kubwa kiasi gani? Hamasa kwa wananchi na Taifa zima ndio hamasa kwa wachezaji pia na wala lengo si Wema, MwanaFa, JB n.k kuhamasisha wachezaji ila nguvu yao mitandaoni ambayo nguvu yake ndio kila kitu zama hizi itahamasisha wananchi wengi wanaowafatilia!!! Vitu vidogo tunataka kutumia nguvu kubwa bila sababu.
Kesho tukutane Taifa kusaidia hamasa na kuwa sehemu ya historia mpya ambayo wapo wengi waliyoitamani kama akina supercoach Mziray lakini hawakuiona na Mungu anatupa fursa ya kuwa sehemu ya historia ambayo mara ya mwisho kuwekwa ni miaka 39 iliyopita.
Yote kheri mpaka sasa ...twendeni Taifa Watanzania lawama angalau zianze Jumatatu!
Sent using Jamii Forums mobile app