Uzalendo kwanza; Lazima tuwe na muda ambao tunaongea lugha moja kama nchi

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kesho Taifa linaingia vitani kwenye soka kusaka heshima, na kujiweka kwenye ramani mpya ya ulimwengu wa michezo duniani kwa kufuzu Afcon.

Tunapokuwa kwenye nyakati kama hizi kitaifa ni vizuri tukawa kitu kimoja na kuelewana kwenye malengo ya kuhakikisha timu ya Taifa inashinda.

Nimeona lawama kwa kamati ya kuhamasisha kutumia wasanii mbalimbali kuhamasisha watanzania badala ya kutumika wachezaji wa zamani na waandishi wa habari za michezo wa zamani.

Sikatai umuhimu wa hao legends kuhamasisha lakini lazima tukubaliane tume target kundi gani. Ile press ya akina Manara na maudhui yote yalikuwa kuhamasisha wananchi kuujaza uwanja wa taifa ili kusaidia kuhamasisha timu.

Nimeshuhudia wachezaji wa zamani akiwemo akina Peter Tino wakiitwa kwenye kambi ya timu ya taifa kuongea na wachezaji na ushawishi na umuhimu wao mkubwa upo huko. Lakini swala la kutangaza na kuhamasisha wananchi kwa zama zetu hizi za mitandao lazima utatumia vijana wenye influence kwasasa.

Tuache kulalamika hadi kwenye nyakati ambazo tunapaswa kuwa kitu kimoja. Inasikitisha sana tunaacha kuhamasishana na kuanza kuandika makala ndefu za lawama kwa watu ambao wanafanya kwa nia njema.

Tuchukulie mfano mdogo, Haji Manara amefanikiwa kuinfluence wana Simba kuujaza uwanja wa Taifa na kuwa chachu ya ushindi kwa mechi za hapa nyumbani. Vipi akiungana na stars wengine kuhamasisha wananchi, hamasa itakuwa kubwa kiasi gani? Hamasa kwa wananchi na Taifa zima ndio hamasa kwa wachezaji pia na wala lengo si Wema, MwanaFa, JB n.k kuhamasisha wachezaji ila nguvu yao mitandaoni ambayo nguvu yake ndio kila kitu zama hizi itahamasisha wananchi wengi wanaowafatilia!!! Vitu vidogo tunataka kutumia nguvu kubwa bila sababu.

Kesho tukutane Taifa kusaidia hamasa na kuwa sehemu ya historia mpya ambayo wapo wengi waliyoitamani kama akina supercoach Mziray lakini hawakuiona na Mungu anatupa fursa ya kuwa sehemu ya historia ambayo mara ya mwisho kuwekwa ni miaka 39 iliyopita.

Yote kheri mpaka sasa ...twendeni Taifa Watanzania lawama angalau zianze Jumatatu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi timu yenyewe inayoenda front imejiandaaje kabla ya sapoti yetu!? Isije kuwa Lipuli inajiandaa kufia uwanjani na Barcelona eti kwa sababu wapo uwanja wa Samora.
 
Ni timu ya Taifa hivyo kati ya watanzania milioni 55 tumempa jukumu kocha achague wa kutuwakilisha. Tuwaunge mkono na kama lawama angalau zianze jumatatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasiasa hawa wababaishaji wakikaa pembeni sina shaka kila mtu ataiunga mkono timu ya Taifa. Lakini wanapoingia watu wachafu kama kina Makonda na vyangudoa professionals kuwekwa viti vya mbele watawakimbiza watu wengi. Na mwisho tuache kujidanganya. Tanzania mpira wa miguu bado kabisa. Kinachotokea sasa hivi ni kama saa mbovu inavyokuwa sawa muda fulani!
 
Mkuu hakuna aliyemkamilifu, tuhamasishane kila mmoja kwa influence yake. Huu ni wakati wetu kama Taifa pamoja na mapungufu yetu. Tuachane na hayo tuhamasishane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hakuna aliyemkamilifu, tuhamasishane kila mmoja kwa influence yake. Huu ni wakati wetu kama Taifa pamoja na mapungufu yetu. Tuachane na hayo tuhamasishane.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mapungufu na makusudi. Tutofautishe. Kuunga mkono kitu ambacho mshenzi kama huyo amejipeleka mbele ni kuunga mkono ujinga wake. Tujaribu kujenga picha kubwa. Ujinga wa kusema ''kila mtu ana mapungufu'' ndiyo umefanya nchi nyingi za kiafrika zibaki nyuma. Tusiunge mkono chochote mtu mhuni kama huyo anachojiweka kimbele mbele full stop. Kutatoa funzo wa wengine wenye nia ya kufanya uhuni kama wake.
 
Achana nae, just focus kwenye timu ya Taifa. Fanya kitu kwaajili ya hilo mkuu. Kwanini ukubali kupoteza nafasi yako kwenye Taifa kwasababu ya mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana nae, just focus kwenye timu ya Taifa. Fanya kitu kwaajili ya hilo mkuu. Kwanini ukubali kupoteza nafasi yako kwenye Taifa kwasababu ya mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una hulka na Roho ya Utajiri kamwe hufikirii Uchawi na Roho mbaya mkuu. Kama sio sasa ipo kesho yako utakuja toboa mbaya. Keep it Mkuuu.
Tanzania ni yetu sote daima tuipiganie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…