Mara kwa mara watu binafsi, taasisi za dini na za kiraia na viongozi wetu wa kisiasa wanekuwa wakituasa watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yetu, japo wengi waneshindwa kutofautisha kati ya nchi na serikali.
Leo mimi nataka niongelee uzalendo kwenye uchaguzi huu ili kuitekeleza dhana nzima ya uzalendo kwa nchi yetu.
Licha ya uchaguzi huu kushirikisha wagombea kutoka vyama tofauti tofauti, ninatamani wagombea wetu waonyeshe uzalendo wao kwa nchi yetu kabla na baada ya matokeo ili kuepusha nchi kuingia kwenye vurugu zisizokuwa na maana.
Pamoja na ukweli kwamba ni jambo la kawaida kwa timu kutaka kushinda mchezo lakini baada ya dk 90 matokeo yanapokuwa kinyume cha matarajio basi timu ikubaliane na hayo matokeo ili mradi mchezo ulikuwa fair.
Vivyo hivyo kwa wagombea wetu ningependa kuwasikia kuanzia sasa kwamba watakuwa tayari kuyapokea matokeo yoyote baada ya uchaguzi hata kama yatakuwa kinyume na matarajio yao.
Hapa ninaiomba sana tume ya uchaguzi ambayo ndio refaree wa mchezo kuhakikisha inachezesha mchezo kwa haki ili mshindi halali wa huu uchaguzi apatikane.
Pamoja na kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye kipindi hiki cha kwanza tume wajitahidi kuzirekebisha hizo kasoro ili kipindi hiki cha pili tuweze kuona mchezo mzuri.
Jeshi la polisi na viongozi wengine wa vyombo vya dola ambao nao ni kama vibendera wa mchezo nao wasimame kwenye haki bila kupendelea timu au mchezaji yeyote.
TAFADHALI WAGOMBEA TUTANGAZIENI KUWA MKO TAYARI KUYAKUBALI MATOKEO YOYOTE HATA KAMA NI KINYUME NA MATARAJIO YENU.
Maana sisi wapiga kura ndio waamuzi wenu.