Uzalendo na wazalendo katika historia ya TANU

Uzalendo na wazalendo katika historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
UZALENDO NA WAZALENDO KATIKA HISTORIA YA TANU: SAFINA YA MAARIFA IBN TV

Nimetembelewa na Mtangazaji wa IBN TV Hemed Lubumba kwa mahojiano kuhusu wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Katika mazungumzo yetu nimetoa historia ya wazalendo wengi wake kwa waume ambao walifanya makubwa katika kupigani uhuru wa Tanganyika lakini hawatambuliki.

Mtangazaji Hemed Libumba alivutiwa sana na historia ya Idd Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa Aljamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mweka Hazina wa TANU.

Idd Faiz Mafungo ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu UNO 1955.

Nimeweka hapo picha mbili ambazo Idd Faiz Mafungo yuko na Nyerere picha ya kwanza ni Idd Faiz ni huyo wa kwanza kushoto na picha ya pili ni huyo mkono wa kulia wa Nyerere.

Picha hii wanamuaga Mwalimu safari ya kwanza UNO 1955.

Hafla ya kumuaga Mwalimu ilifanyika katika jengo la shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lilikokuwa New Street kona na Mtaa wa Aggrey.

Screenshot_20220131-182250_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom