Uzalendo ndio huu, Dar-New York kwa B787-8 gharama ya mafuta ni TZS 267M

Mama wa kimataifa,
 

Ulichokosea kwenye hesabu yako (nadhani ni kwa makusudi) ni kuwa haiwezekani msafara wa Rais kukatiwa tiketi ya economy class!! Diplomatic personnel wote hawatuumii economy class!! Hapo iliyotumika ni First Class ambayo Bei yake ni karibu Mara mbili ya economy class!!
Ukifanya téna hesabu kwa kutumia first class utakuta kwamba hakuna unafuu wowote wa maana. Ukizingatia risk ya usalama ndio kabisaa ni hasara kutumia ndege za mashirika ya nje. Angetumia ndege ya shirika letu tungesema pesa zimebaki kwetu !! Hapo hakuna kitu, zaidi ya AIBU!!
 
Ni kweli aisee ila hawana aibu!
 

Asante Sana. Umemaliza Kila kitu!!
 
Umewahi kukata group tickets kwenye mashirika ya ndege au unatomboka tu?
First Class Haina lugha ya group ticket!! Hiyo lugha ya group ticket ni huko economy class!! Achana na habari ya first class!! Ukilia Lia unaambiwa hustahili first class!! Kajichanganye huko kwa walala hoi economy class!
 

Beberu akikusifia ujue umepigwa!! Beberu akisifia mazingira mazuri ya uwekezaji, ujue kaona shamba la bibi!!
Ndio maana mabeberu hayawezi kuisifia China, Urusi, Cuba, nk. Maana huko hakuna shamba la bibi!!
Ukiona mama anasifiwa na mabeberu, si dalili nzuri!! Tanzania inawindwa Sana!!
 
Unajua Rais Samia amejenga madarasa elfu 18?

Endelea kumwombea
Madarasa hayo yamejengwa kwa mkopo wa corona ambao utalipwa kwa Kodi za watanzania ! Kwa hiyo madarasa hayo yamejengwa na watanzania! Kwa taarifa yako mshahara wa Rais haukatwi Kodi!! Kwa hiyo si miongoni mwa waliojenga, Japo amehusika katika upatikanaji wa mkopo kwa dhamana tuliyompa sisi watanzania. Ni mtumishi wetu na 2025 atatuomba kura!
 
Je, Mama kaenda na ya abiria au ATCL?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…