Uzalendo, utakulinda

Mbelajr

Member
Joined
Sep 14, 2018
Posts
14
Reaction score
6
Wanabodi salaam! Neno uzalendo limekuwa likizungumzwa sana hasa na wanasiasa lakini hatupaswi tu kuwaachia watu wa tabaka moja kuzungumzia Jambo hili.Uzalendo NI zaidi ya UTAIFA,Kila Mtu ataungana na Mimi kwamba ukiachana na nchi yako uliyozaliwa hakuna nchi nyingine yoyote unayoweza kwenda kuishi kwa uhuru zaidi ya nchi yako ya asili

Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa kuipenda nchi yangu.Kuwa tayari kwa wakati unaofaa na usiofaa kuilinda na kuitetea.

Ndugu zangu Watanzania hivi karibuni kuliibuka sintofahamu ya watu wasiojulikana.Karibia Kila Kona ya nchi msamiati huu ulienea.Kwa mfano Kupotea kwa Been Saanane,Azory Gwanda na Kupigwa Risasi kwa Mwanasiasa Tundu Antipas Lissu.Matukio haya yote yalitolewa nadharia kuwa yamefanywa na watu wasiojulikana.Naam nami nasadiki ni Watu wasiojulikana,lakini watu waliofanyiwa matukio haya ni watu wanaojulikana.Je Hawa watu wanaojulikana shughuli zao hasa NI nini? Nitatoa mfano wa Mtu mmoja,Tundu Lissu.

Tundu Lissu ni Mwanasiasa machachari kutoka kambi ya upinzani,mpaka tukio Lile linampata Taifa letu tukufu lilikuwa likipita Katika wakati mgumu wa kutetea raslimali zetu zilizokuwa zikiporwa na mabeberu.Hili si jingine NI sakata la makinikia.Je Tundu Lissu alikuwa upande gani?

Upande wa mabeberu au upande wa Taifa letu(UZALENDO)? Katika namna yoyote ile unapocheza na maslahi ya Taifa NI ngumu kubaki salama. Naomba ieleweke kuwa Siungi mkono shambulio la ndugu YETU Tundu Lissu kwa namna yoyote ile.Ninachojaribu kusisitiza unapokuwa mzalendo Taifa litasimama na wewe kwa gharama yoyote ile.Watanzania tuwe makini na mabeberu tusije kutumika kuvuruga amani na ustawi wa Taifa letu.

Nimalize kwa msemo huu "Kuwa mzalendo Ni kukubali kuwasaliti maadui wa Taifa lako,Ukiwachokoza watu wasiojulikana utapata tabu saana" Nawasilisha!¡
 
Dogo kwa iyo unataka kusema huyo mwanasiasa alishambuliwa na serikal ? Maana umesema huwez kua upande wa pili ukabaki salama? Ww una elimu gan kwanza ? Una maana lissu alivyo sema kua tutashtakiwa kwa kuvunja Mikataba ambayo sisi ni members wake kama Mega ndo anakua adui? Unajua hii kesi tutashndwa vibaya Sana? Alivyo sema ndege yetu imekamatwa ndo alibadilika kua adui wa taifa? Nan adui wa taifa kati ya alyetuambia dege letu kimekamatwa baada ya kushndwa kwenye kesi ya kuvunja Mikataba ya kimataifa ovyo pasipo kufuata taratbu? Kwanza umekula Leo maana naisi hujala? Pili huna ulicho andka kama ww ni mmoja wa vijana wa taifa ili basi tutakua na taifa vivu sana kufkir baada ya miaka 20-30 ijayo.
 
Hahaaaa mkuu ahsante kwa hoja zako ulizoziibua kwa njia ya maswali.Tumuombee TL afya yake iimarike arudi nyumbani tuje tulijenge Taifa kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…