Uzalendo Wamsinda Mlokole

Uzalendo Wamsinda Mlokole

PJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
297
Reaction score
32
Bwana mmoja ambaye ni Kiwete alienda kwenye mahubiri ya Mhubiri mmoja wa kimataifa kwa ajili ya kutafuta uponyaji.

Siku moja Bwana akamkumbuka na kumponya akawa mzima akatembea. Akasimama mbale ya jukwaa na kutoa ushuhuda jinsi Mungu alivyomponya na kusema tangu siku hiyo ameokoka na kuwa atamtumikia Bwana peke yake.

Siku moja mlokole huyo alipokuwa katika usafiri wa daladala (DCM) amesimama huku kakamata bomba mbele yake kulikuwa na binti mmoja mrembo sana na kajaza kisawasawa. mara jamaa kaanza kumtamani yule binti na kuwaza namna atakavyompata ili akavinjari nae na kusahau kuwa aliambiwa enenda zako usitende dhambi tena!!

Kufumba na kufumbua jamaa kajikuta ile hali ya zamani ya kuwa kiwete imemrudia na ananing'inia kwenye bomba la DCM huku miguu haiwezi kufika chini. akaanza kupiga kelele kuomba msaada watu wamshushe asianguke. Watu wote walibaki vinywa wazi bila kujua nini kilitokea. :help:
 
Back
Top Bottom