Stranger94
New Member
- Sep 11, 2022
- 2
- 0
UTANGULIZI
Uzalendo ni neno lenye maana pana inayohusisha mapenzi ya dhati na uwajibikaji kwa nchi yako. Tanzania ni moja kati ya nchi kubwa barani Africa yenye mtaji wa watu zaidi ya milioni 60. Tanzania imejitofautisha na nchi zingine duniani kwa mambo mengi ikiwemo lugha adhimu ya Kiswahili. Nchi nyingi barani Africa zinatumia lugha za wakoloni lakini imekua tofauti kwa Tanzania. Ukarimu na kupenda amani vimekua silaha kubwa kwa Tanzania hususani inapofananishwa na nchi zingine Africa.
TUTENGENEZE VYA KWETU
Tanzania ina uwezo wa kujitangaza zaidi na kutawala kwenye nyanja mbalimbali duniani ikiwemo Muziki, Utalii, Filamu, Michezo kwa ujumla, Madini na Gesi kama ifuatavyo;
MUZIKI; Tanzania imebarikiwa vijana wengi na wenye vipaji vya kutosha hususani vya muziki. Tatizo linakuja kwenye aina ya muziki wanaoimba vijana hao. Tumekua na uraibu wa kuiga aina za muziki za wenzetu hususani kutoka Nigeria na Afrika ya kusini, hii sio sawa. Tanzania tuna muziki wetu ambao tukiamua kuupandisha inawezekana. Ipo wapi Bongo Fleva halisi leo, ipo wapi Taarabu, ipo wapi Singeli na aina zingine nyingi. Kwanini tusichague aina moja ya muziki na kuamua kuiunga mkono kama taifa ili iweze kuwa utambulisho wetu duniani. Afrika ya kusini wamefanikiwa sana katika hili walianza na kwaito tukaiga leo wana Amapiano tumeiga pia. Nigeria wameamua kukomaa na muziki wao na unawatambulisha duniani kote na unawalipa, vipi kuhusu sisi? Ipo haja ya wanamuziki kukaa na kutengeneza aina moja ya muziki utakaotutambulisha duniani na kutupa faida pia.
FILAMU; kiwanda cha filamu Tanzania kimeshindwa kabisa kuteka mioyo ya watanzania kama ilivyokua miaka ya nyuma. Kukosekana kwa umoja na elimu ndio changamoto kubwa kwenye tasnia ya filamu nchini. Vipaji vipo vingi tena kuliko wakati mwingine wowote, zama zimebadilika ila wasanii wakongwe wa filamu bado wanaishi kwenye zama zilizopita. Watanzania wanahitaji ubora na vipaji halisi sio hadithi na wahusika wa kizamani. Baadhi ya filamu kama Jua kali, Huba na nyingine nyingi zimeanza kuonyesha kile watanzania na dunia nzima inachohitaji. Tukiamua kama watanzania tunaweza kuirudisha tasnia hii na kuiteka dunia. Tunaweza tukaona ni ngumu lakini tuchukue mifano kwa nchi kama Korea na Uturuki ambazo hazikua maarufu hapo mwanzo lakini sasa tunazitambua kutokana na filamu zao.
UTALII; dunia nzima inatushangaa kwenye hili, ni kipi tumekosa kwenye sekta ya utalii?. Tanzania imebarikiwa mbuga za wanyama na hifadhi za taifa kubwa, nyingi na zenye kuvutia. Tuna mlima mrefu zaidi Afrika (Kilimanjaro), tuna fukwe za kipekee kabisa, na vivutio vingine vingi. Leo nchi kama Kenya inatuzidi kwenye utalii, hakika tunapaswa kuona aibu, leo Rwanda inakuja juu kwenye utalii kutokana na uwekezaji wao, hapa tujicheke kidogo. Mafanikio huja kwa gharama na kwa leo wanaojitoa, sekta hii inahitaji uwekezaji ambao sio mkubwa sana kwasababu vivutio vyenyewe vinajiuza. Nimpongeze raisi wa awamu ya Sita mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizoziweka kwenye filamu ya Royal tour, hakika tumeanza kuona matunda yake. Tukiwekeza vizuri kwenye sekta hii basi nusu ya patola taifa itatokana na sekta hii.
MICHEZO; hapa ndio kuna kitendawili kigumu zaidi. Ipo michezo ambayo tunafanya vizuri hususani masumbwi ambayo inahitaji jitihada binafsi lakini linapokuja suala la timu hapo ndipo kitendawili kilipo. Sio rahisi kuamini kama nchi yenye watu zaidi ya milioni 60 inashindwa kupata watu 11 wa kuliwakilisha taifa kwenye mpira wa miguu. Siasa za mpira ni changamoto kubwa Tanzania, ni kweli na ni vizuri tunavyozipenda Simba na Yanga lakini mapenzi hayo tuyahamishie pia kwa timu za taifa, leo timu ya taifa haifanyi vizuri kutokana na siasa za Usimba na Uyanga. Tuwekeze kwenye riadha kuna vipaji vingi nchini. Ipo haja ya kuifanya michezo kuwa somo rasmi kuanzia shule za msingi mpaka elimu ya juu.
MADINI NA GESI; mwanzoni mwa miaka ya 90 Umoja wa Falme za Kiarabu ulikua ni nchi ya kawaida ya jangwani lakini itazame leo baada ya miaka 30 pekee. Hii imetokana na raslimali ya mafuta ambayo imewafanya watajirike. Leo hii wanafanya vizuri kwenye utalii, biashara na utafiti wa anga. Kila mmoja wetu anatamani kutembelea Dubai lakini miaka 30 nyuma ilikua ni jangwa lililojaa vumbi. Tanzania imebarikiwa madini ya aina mbalimbali kama vile Dhahabu, Almasi, Uranium, Tanzanite na mengine mengi kila kona ya nchi, lakini sekta ya madini haina mchango mkubwa kwa taifa kama ilivyotarajiwa. Tanzanite inapatikana Tanzania pekee, hakuna nchi nyingine duniani yenye madini hayo. Tuna gesi lakini bado tunapika kwa kuni lakini pia hata bei ya gesi nchini ni kubwa kama vile inatoka nje. Serikali itengeneze sera na mikataba bora ya madini na gesi kwa maendeleo ya taifa, tuache siasa kwenye mambo ya kitaifa.
HITIMISHO
Yote haya yatafanikiwa na kuleta tija kwa nchi endapo yatafanyiwa kazi vizuri. Hizi ni sekta ambazo zinaweza kuzalisha ajira nyingi nchini na kuondoa tatizo la ajira nchini. Kumekua na changamoto ya ajira nchini (Rejea andiko langu TATIZO LA AJIRA TANZANIA, NINI KIFANYIKE?), changamoto hii inaweza kupunguzwa kwa angalau asilimia 50 na sekta hizi endapo tutaamua kuwa wazalendo kwa nchi yetu. Uwekezaji unahitajika ili kuufanya uchumi wa taifa usitegemee kilimo na ufugaji ambao pia tumekua hatufanyi vizuri. Viongozi tunaowachagua wanapaswa kuwa wazalendo na wawajibikaji kwenye nafasi zao ili tuweze kuifikisha nchi yetu pale tunapotamani ifike. Natamani siku moja iwe nchi maarufu duniani kutokana na rasilimali na watu wake.

Upvote
0