Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Utoaji wa gesi ukaa ulipungua mwaka 2020.
Ripoti mpya iliyotolewa na wanasayansi wa Ulaya imesema utoaji wa gesi ya ukaa kutokana na matumizi ya makaa ya mawe, mafuta ya petroli na gesi asili umepungua kwa asilimia 7 mwaka 2020 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Data zilizokusanywa zinaonesha kiwango cha utoaji wa gesi hiyo chafuzi ulipungua kwa asilimia 12 nchini Marekani na asilimia 11 kwenye kanda ya Umoja wa Ulaya.
Waatalamu hao wamesema janga la Virusi vya Corona limechangia kwa kiasi kikubwa mwenendo huo kutokana na kupungua kwa matumizi ya nishati chafuzi baada ya kufungwa kwa shughuli nyingi za uzalishaji duniani.
Hata hivyo tayari kuna wasiwasi kuwa utoaji wa gesi ukaa utaongezeka tena mwaka 2021 katika wakati mataifa duniani yaendelea na juhudi za kuchochea ufufuaji uchumi ulioathriwa na janga la virusi vya coorna.
Chanzo: DW Swahili