Uzalishaji wa vyakula vya mifugo umeongezeka kwa kiasi kikubwa Tanzania chini ya serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Joined
Aug 11, 2024
Posts
54
Reaction score
24
Uzalishaji wa vyakula vya mifugo vilivyosindikwa viwandani umeongezeka kutoka tani 900,000 mwaka 2020 hadi tani 1,880,000 mwaka 2024.

Aidha, ongezeko hili limetokana na Serikali kuendelea kuhamasisha na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa Sekta Binafsi ili kukabili ongezeko la mahitaji ya vyakula vya mifugo.

Vilevile, viwanda vipya 51 vya kuzalisha vyakula vya mifugo vimesajiliwa katika Mikoa nane (8) ya Arusha (9), Kilimanjaro (3), Dar es Salaam (16), Morogoro (4), Mwanza (1), Katavi (1), Dodoma (1), Iringa (3), Mbeya (1), Pwani (10) na Shinyanga (2) na kufanya viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo kuongezeka kutoka 199 mwaka 2020 kufikia 250 mwaka 2025.

Pakua Samia App kupitia Play Store au App Store
 
Sizani kama kuna ubaya katika hili kama ikiwa Serikali anayoisimamia imefanya makubwa haya kwenye sekta ya kilimo.
Ukubwa upi? yaani unaona sisi wafugaji wa ng'ombe kununua kenya ndo kupiga hatua? vifaranga kutoka 1200 hadi 2200 ndo hatua? kwanini wasiruhusiwe wakenye kuingiza vifaranga wao nchini?
 
Hio ni Bei ya kununua, vipi bei ya kuuza nayo imepanda au imebaki Ile Ile?.
 
wakenya kuzuiliwa sio sawa kwani sio wote tuna mtaji wa kutosha bado sana tunajikongoja na uhitaji ni mkubwa. wee angalia unatoa oda mwezi mzima ndo unapata vifaranga wamewahisana wiki2
Ndio nasema watu wenye mitaji watumie hio kama furusa, Bado vifaranga wakijaa mtaanza lalamika masoko yakuuzia, na mtakuwa mnauza kwa Bei za hasara kwa sababu hamtoweza shindana na wakenya wenye mitaji mikubwa.
 
ukiruhusu uingizwaji kiholela ni hatari sana mfamo majuzi hapa kuna vifaranga vilipenya toka kenya vimeharibu sana bei ya kuku.japo kwa sasa naona hali ni shwari
 
Najua lakini wazarishaji wa ndani ndo kama hivyo mara wazarishe au waache tu jiulize kifaranga kutoka kwenye 1200 hadi1800 na wengine wanauza hadi 2200 kwa sasa wee unadhani ni sawa ?bei wanajipangia tu. chakula hadi95k kwa kg50!
 
Ndio nasema watu wenye mitaji watumie hio kama furusa, Bado vifaranga wakijaa mtaanza lalamika masoko yakuuzia, na mtakuwa mnauza kwa Bei za hasara kwa sababu hamtoweza shindana na wakenya wenye mitaji mikubwa.
Nini kifanyike ili kurinda soko la ndani na pia wafugaji(wanunuzi wa vifaranga) tusipate adha ya kusubiri muda mrefu na wakati mwingine hupati kabisa?
 
Uzalishaji wa vyakula vya mifugo vilivyosindikwa viwandani umeongezeka kutoka tani 900,000 mwaka 2020 hadi tani 1,880,000 mwaka 2024.

Aidha, ongezeko hili limetokana na Serikali kuendelea kuhamasisha na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa Sekta Binafsi ili kukabili ongezeko la mahitaji ya vyakula vya mifugo.

Vilevile, viwanda vipya 51 vya kuzalisha vyakula vya mifugo vimesajiliwa katika Mikoa nane (8) ya Arusha (9), Kilimanjaro (3), Dar es Salaam (16), Morogoro (4), Mwanza (1), Katavi (1), Dodoma (1), Iringa (3), Mbeya (1), Pwani (10) na Shinyanga (2) na kufanya viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo kuongezeka kutoka 199 mwaka 2020 kufikia 250 mwaka 2025.

Pakua Samia App kupitia Play Store au App Store
View attachment 3179453
Serikali ndio inawasiadia kuzalisha au wanapambana wenyewe ikiwemi kuhabga hadi kuoata vibali? acha ujjinga
 
Back
Top Bottom