UZALO.. Friday. 11 Jun.
Xulu akiwa na mkewe wanataniana kidogo kuhusu mambo yao jikoni, mkewe anagusia swala la xulu kwenda wote kanisani familia nzima kwa nia ya kumuaga kijana wao mxolisi anayerudi joburg kufanya kazi..
Pastor mdleshe na mkewe pamoja na mtoto wao nkosinathi, wakijiandaa kwenda kanisani huku wakimsubiri ayanda aliyekwenda mazoezini.
Njiani ayanda akiwa anarudi kutoka mazoezini huku akikimbia anamparamia sindi, kisha anamuomba samahani na kuendelea na Safari,
Sindi anakutana na kijana mmoja na kumuulizia ni wapi kwa pastor mdleshe ili akatoe ukweli kuhusu watoto wawili ayanda na mxolisi kuwa walibadilishwa na na mama yake alipokuwa nesi miaka ya 90, hivyo ayanda ni mtoto wa xulu na si pastor mdleshe na mxolisi ni wa pastor na sio xulu.
Mastermind baada ya kulikoroga anakutana na mfanyakazi mwenzie wa gereji kisha anampanga kuwa watamfute sbu na kumuua kwani ni snitch anashirikiana na polisi, kutoa taarifa zao, lakini anamuonya jamaa huyo kuwa asimwambie mtu
Sindi anafika nyumbani kwa pastor na kukaa sana getini hadi anapopita mamlambo anayesali kanisani kwa pastor na kumwambia sindi kuwa pastor na family yake wamekwisha kwenda kanisani hivyo kama ana shida naye waende kanisani huko huko atampata, wanaondoka.
Kanisani kwaya inaimba kabla ya ibada sindi anaelekezwa kwa pastor, lakini pastor yuko bize na ibada inaanza,anaambiwa amfuate pastor baada ya huduma kisha pastor anakuja kutoa neno kidogo
Sbu anaonekana akila unga wake (cocaine)
Inspector dhlomo anampigia sbu simu na kumwambia achague lililo jema either waendelee kufanya kazi au arudi jela
halafu anaacha kwaya iimbe tena kisha anaanza kutoa neno,
Kisha anaomba ushuhuda au kwa wenye kutubu, hapo anasimama mke wa xulu na kwenda kwa mbwembwe sana na kuanza kusifia pesa zao familia yao na kuanza kumsifia kijana wake mxolisi kuwa ana akili hajawahi kuwa hata wa tano ila anakuwaga wa kwanza au wapili ππ
Watu wanaonekana kuboreka.
Kisha kwa mara nyingine tena pastor anauliza kama kuna mwengine basi anasimama sindi kisha anaenda mbele na kujitambulisha kuwa ni mgeni, anasema kaja kutoa ukweli ambao anajua utawaumiza wahusika lakini ndio njia pekee ya kuujua ukweli.kisha anaenda kukaa kwanza
Kwaya inarudi tena kuimba.
Wakiwa hapo kanisani ghafla anaingia sbu akiwa kachafuka usoni koti liko wazi anafyatua risasi tatu akiwa na bastora mkononi, zinaskika kelele humo ndani
Mpka jumatatu hiyo..