Uzalo Special Thread

Naona kaka wa Xulu ndio mafia zaidi
Kampa mbata ya haja Ayanda[emoji2]
ayanda kajifanya mnoko likamuweka moja tu kaenda kukandwa na mama yake
Hili jamaa na kaka ake inaonekana haziivi.
 
ayanda kajifanya mnoko likamuweka moja tu kaenda kukandwa na mama yake
Hili jamaa na kaka ake inaonekana haziivi.
Hahhaa halafu nahisi huyu ndio alikuwa anampigia xulu simu wkt yupo jela
Halafu kama anammendea shemeji yake
 
Hahhaa halafu nahisi huyu ndio alikuwa anampigia xulu simu wkt yupo jela
Halafu kama anammendea shemeji yake
eeeh ndio huyu siku ile kwa simu alikuwa anaita brother..
Any update kwa jana walioangalia?
Halafu lilisema eti vipi yule mkeo mwenye chura yupo?
 
Katika mazoezi ya kwaya mama mchungaji apendekeza itafutwe sauti ya kiume ambayo itakuwa ikiimbwa pamoja na sauti ya Nombuso katika kuongoza kwaya,GC ajitokeza na kujipendekeza yeye ana sauti nzuri na kujaribu kuimba lakini anakataliwa.
 
Katika mazoezi ya kwaya mama mchungaji apendekeza itafutwe sauti ya kiume ambayo itakuwa ikiimbwa pamoja na sauti ya Nombuso katika kuongoza kwaya,GC ajitokeza na kujipendekeza yeye ana sauti nzuri na kujaribu kuimba lakini anakataliwa.
eeh vipi xulu na kaka yake?
Hilo li GC linaboa
 
Nkosinathi akiwa anapiga story na baba yake,ampongeza kwa kuwa shujaa,na kusimamia kile anachoamini tofauti na watu wengine kwa kuwa ni waoga,amuaga baba yake anaenda kumuona Amandla.
 
Mdogo wake Xulu amtania shemeji yake,wakiwa jikoni na kumkumbusha enzi hizo wakiwa shule,wakumbushana wimbo wa enzi zao na kuanza kucheza pamoja,Xulu awashuhudia na bdae kuwashitua na kuonesha kutopendezwa na lile tukio.
 
Mdogo wake Xulu aona 'gari ya kifahari kijerumani' ikiwa inatengenezwa kurudishiwa upya wake,amuuliza kwa mbwembwe kaka yake gari ni ya nani,aambiwa ni yake,anafurahia sana,anapewa na kibunda cha pesa na Xulu na kuambiwa katafutiwa na nyumba ya kuishi,lakini Xulu anamuomba favour mdogo wake,kuwa 'akae mbali na mke wake'.
 
Nombuso amkuta Mxolisi akiimba, ashangazwa na sauti nzuri ya Mxo,na kumsifia sana,pia anamwambia kafurahi kumpata mwanaume atakayeimba naye kwenye kwaya na kumuomba Mxo aungane nae,wawe wanaimba pamoja kwenye kwaya,Mxo anasita na badae kukubali.
 
Mama mchungaji akiwa na Ayanda na Nombuso...ashangazwa kutomuona Nkosi nyumbani mida ile,ayanda anajaribu kupiga simu ya Nkosi na kushangaa kutopokelewa,Nkosi baada ya kuonana na Amandla,akiwa anarudi na kupita 'panelbeaters' ashangazwa na kuona mastermind akiingia panelbeaters akiwa na gari kali range rover,naye akaingia kwa kunyatia na kuonesha kushangazwa na jambo na kuziba mdomo,Xulu akamfuata kwa nyuma kwa kunyatia na kumkaba roba kali na uzalo ikaishia hapo...
 
Dah xulu mtihani anao si kwa kivuruge huyo...Namuonea huruma sana pastor anapitia kipindi kigumu mda huu,izo bili nahisi kama xulu anahusika (sina uhakika)
 
Wakuu Week lote nilikuwa beneti
Naskia mxo kampiga denda nombuso?
Na vipi mkontho ana mpya gani?
 
Naskia mxo kampiga denda nombuso?
Nombuso anaoneka wazi anampenda mxolisi na Ayanda hana chake pale jamaa alifanya kosa kubwa akimuacha Nkule.
Na vipi mkontho ana mpya gani?
Mkontho inaonesha ametokea kukapenda kasister kake na Mastermind japo hajakaaimbia pia Xulu alimwambia mkontho akamuue mtoto wa mchungaji hospitalini akakataa sasa Xulu ana-mfremu ndugu yake kwa mara ya pili ili arudi gerezani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…