Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,158
- 4,449
Wakuu naomba ushauri, nina mtoto wa mwaka mmoja na miezi Miwili na mipango yetu ni kuwa na watoto wawili tuu Mungu akipenda, na tulipendelea wasipishane sana umri, ili tumalize mambo ya uzazi tuendelee na mambo ya ulezi na Shughuli nyingine. lakini kwa bahati nzuri au mbaya huyu first born wetu alipatikana kwa njia ya operation, je kiafya kwa umri huu wa mtoto yaani miezi 14 ni sahihi kwa mama yake kushika ujauzito mwingine???. Nishaurini kistaarabu ushauri wenu nitaufanyia maamuzi.