Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Natamani nikifikisha miaka 60 kama Mungu atajalia, nisiwe natumia nguvu nyingi sana za kupata ugali kwa siku. Kama itawezekana, uwe ni umri wa kucheza na wajukuu pamoja na kwenda kuwinda au kushangaa kobe porini.
Siku ya ibada kwa sababu mimi ni mkiristu, nisiwe nasali katika kanisa moja, bali kila jumapili niwe naenda kusali kanisa jingine.
Niwe nakula vyakula vya asili na kwa upande wa nyama niwe nakula nyama pori kama za sungura, ndege, swala, samaki n.k
Nitapenda niwe na dreva wa kike ambaye atakuwa smati na mcha Mungu, ambaye tutakuwa tunaenda naye tripu mbalimbali; nimechagua wakike kwa sababu ili safari zisiwe zinanichosha.
Nitapenda muda mwingi niishi porini ili niweze kupata hewa safi ambayo haijachakachuliwa na uharibifu wa mazingira.
We uzee wako unataka uweje?