Uzee wako unataka uweje?

Mleta mada ili ufikie ndoto zako katafute shamba ekari 20, Anza kujenga miundombinu ya mifugo Sasa na kupanda miti ya matunda. Ukisubiri kufanya maandalizi baada ya kustaafu haitawezekana.
 
Aaahahhahahaaa daah...!

Imebidi nicheke, ngoja nimuulize babu Asprin

Eti big Sam, unamfahamu jibibi Shangingi Kasinde?? 😆😆😆
 
Inawezekana kabisa, umeweka mikakati gani ili kufikia hayo malengo?
 
Mleta mada ili ufikie ndoto zako katafute shamba ekari 20, Anza kujenga miundombinu ya mifugo Sasa na kupanda miti ya matunda. Ukisubiri kufanya maandalizi baada ya kustaafu haitawezekana.
Naichukua hii pointi mkuu kwa utekelezaji
 
Kwa hali ilivyo sijui itakuaje nikiwa na umri huo,sijui nitaendelea kuzichakata kama kawaida! Au ndio nitakuwa nishajichokea Mungu ndio anajua
 
Niwe nimeandaa miundombinu ya kuniingizia kipato cha kuweza kunihudumia Mimi na kuweza kuendelea kutoa sadaka na misaada kwa wanaohitaji

Naogopa kufikia umri huo huku nikiwa bado kapuku kiasi cha kuwatolea watoto maneno ya laana kila wanapokosa kukutimizia

Nibaki na moyo na Ari ya kufanya ibada,pia niweze kuchachua siku moja moja na nisichague mavazi
 
Wazo nzuri, ni mikakati gani ambayo tayari umeshaanza kuitekeleza?
 
Nimeshajenga himaya ya kibiashara japo haijafikia uwezo ninaouhitaji .....na Nina waandaa watoto wawe wasimamizi na waendelezaji wazuri ktk siku ambazo nitalazimika kung'atuka
Vizuri mkuu, kama umeanza kuchukua hatua za mwanzo ni rahisi kuja kufanikisha lengo
 
Mleta mada ili ufikie ndoto zako katafute shamba ekari 20, Anza kujenga miundombinu ya mifugo Sasa na kupanda miti ya matunda. Ukisubiri kufanya maandalizi baada ya kustaafu haitawezekana.

Namshukuru Mungu hapo nilishalifanyia kazi hilo ekari zipo na nimeishapanda matunda aina nyingi tu na kanyumba kadogo kwa ajili ya muangalizi kwa muda na kwa mkataba pia ili asije akalazimisha iwe kwake maana hawachelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…