MR KUO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,678
- 3,818
Kipindi cha awamu ya chuma,jiwe tulishuhudia huduma bomba sana kwa watumishi wa umma ngazi zote, kuanzia chini hadi juu, ila baada ya kuondoka inaonekana kaondoka na vyote mapanya buku yametawala baada ya paka kusepa.
Majuzi hapa nilienda shule x kuomba nafasi ya uhamisho kwa kijana wangu wa kidato cha kwanza, nikaonana na mkuu wa shule nikajieleza shida yangu vema, yeye akaniambia hapa nafasi hakuna kabisa jaribu shule ya jilani hapo na alirudia zaidi ya mara 5 kunielekeza kwenye hiyo shule huku akiisifia hadi nikapata mashaka, ila kwa sababu mimi nilikuwa nimeona panapomfaa kijana ni pale pale nikaomba anifanyie vyovyote kijana ahamie, akanitazama kwanza kisha akaniambia sawa nitakusaidia ukitaka aje lipia hela ya dawati, nikauliza sh ngapi akaniandikia kwenye karatasi kiasi cha 120,000/=, nilishtuka ila nikaficha mshituko ikabidi nijifanye naomba huruma akaniambia haiwezekani vinginevyo fanya nilivyokwambia,nikasema kiasi hicho sina kwa sasa,akaniambia kama vipi nije kesho yake ili nionane na fundi wake tuone tunafanyaje ikiwezekana nilipie kwa awamu, kumbe kesho yake yenyewe hatakuwa ofisini kutwa nzima, nilikuja kugundua maana hata mimi nilipata dharula nikaitwa ofisi ya mkurugezi manispaa kwa shughuli zangu,
Ile namaliza naondoka tukakutana nikamsalimia vema tukatoka mazingira ya ofisi nikakumbushia jambo langu na yeye akakomalia kiasi hicho, sasa sijui ikawaje wakati tunaondoka kwa mguu nikapigiwa simu nirudi ofisini, ikabidi nimuage narudi, nikarudi nikamalizana nao ile naondoka pia nikakumbuka si kuna maafisa elimu hapa ngoja niwachek, nikamchek afisa elimu sekondar nikamweleza namna nilivyokwama kutokana na ghalama ya kununua dawati.
Akauliza maswali nikamtajia vyote akashtuka kisha akampigia simu mkuu wa shule, wakaongea kama dakika 20 nikaona hapa huenda nimelipua liziki za watu nikawa na hofu fulani aisee.ile anamaliza kuongea akaniambia amemalizana na mkuu wa shule kesho nirudi shuleni tuelewane anionyeshe dawati ambalo ni bovu nitengeneze mtoto ahamie, kesho yake nikaenda kweli cha ajabu mkuu wa shule akaruka vyote akadai hawajaongea hivyo.dah nilichoka nikajisemea hawa tayari tushapishana kimawasiliano haina haja ya kurudi tena hapa nikaaga na kuondoka.
Napanga kumtafutia shule nyingine ila nimechukia na kusikitika sana.
How come mtu ana shida ya kiofisi na wewe unamwambia njoo kesho siku ambayo unajua hautakuwepo ofisini hivi unafikiria ghalama anazoingia katika muda wake, pesa zake n.k??
Nimechukia sio kidogo.