Ng`wanakidiku
JF-Expert Member
- Apr 18, 2009
- 1,195
- 232
Nasema form four wamefeli kwa haki. Ni uzembe wa wazazi/walezi. Mi nakumbuka kuna mwaka dogo mmoja kanipigia simu toka mikoani anasema eti naomba unipe link za kununua mtihani, na aliamini mimi nilifaulu kwa kuiba mtihani, nilimuambia ukweli sijawahi kununua mtihani na nilipata div one. Ila kwa kizazi cha sasa, unakuta watoto wanajua timu za UK, Hispania, Italy kuliko Yanga na Simba, na movie haswa tamthilia, hii inatokana na wazazi wengi kutokuwa na control za TV majumbani. Tuache ujinga wa kukubali vitu vya kijinga kuwaonea huruma hao waliofeli, tufikiri pia ni uzembe wa vijana wetu na wazazi.