Uzembe tulioulea na tunaoulea ktk Elimu

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2009
Posts
1,195
Reaction score
232
Nasema form four wamefeli kwa haki. Ni uzembe wa wazazi/walezi. Mi nakumbuka kuna mwaka dogo mmoja kanipigia simu toka mikoani anasema eti naomba unipe link za kununua mtihani, na aliamini mimi nilifaulu kwa kuiba mtihani, nilimuambia ukweli sijawahi kununua mtihani na nilipata div one. Ila kwa kizazi cha sasa, unakuta watoto wanajua timu za UK, Hispania, Italy kuliko Yanga na Simba, na movie haswa tamthilia, hii inatokana na wazazi wengi kutokuwa na control za TV majumbani. Tuache ujinga wa kukubali vitu vya kijinga kuwaonea huruma hao waliofeli, tufikiri pia ni uzembe wa vijana wetu na wazazi.
 
50% uko sawa
 
mimi mwanangu wa form two msichana nilimkuta na kipande cha gazeti anasoma 'Kona ya Mahaba'. halafu usiku halali anaongea na simu tu sijui kwenye mtandao unaitwa whatsup. Kusoma vitabu vya kiada na kufuatilia notisi alizopewa na mwalimu shule hataki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…