SoC02 Uzembe wa kufikiri hututoa akiri na kuzaa ujangiri tuimarishe uzalendo

SoC02 Uzembe wa kufikiri hututoa akiri na kuzaa ujangiri tuimarishe uzalendo

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 28, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Ni katika kijiji kidogo kilichopo kusini mwa nchi ya Tanzania ambapo shughuli za kilimo na ufugaji zikiwa ndizo shughuli mama zaidi katika eneo lile ambapo msingi mkuu wa shughuli hizo ukiwa ni ardhi ambapo kwa neema za Mungu eneo hilo lilijaaliwa kuwa na rutuba ya kutosha kwaajili ya mazao ya wananchi wa nchi iliyo tunukiwa kwa karne na karne eneo hilo limekuwa likitumika kufanyia shughuli hizo huku mabadiliko ya hapa na pale yakionekana kujongea katika eneo lile kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu siku hadi siku na hivyo kuleta ushindani katika eneo hilo.

Machweo moja ya utata, alionekana mwenykiti wa kijiji hicho akiranda randa katika ardhi ya mgongo ule akiambatana na wanaume wawili wenye muonekano wa kigeni wenye vitambi vya pesa na suti za uroho, macho yao yakiwa juu juu wakiitolea macho dhahabu ya raia wema wa kijijini hapo.Pande kubwa la ardhi likakatwa na baadhi ya wanakijiji kupunguziwa ama kuchukuliwa kabisa maeneo yao kwa madai ya kwamba maeneo hayo yapo chini ya uangalizi wa sirikali, hivyo wakaombwa kupisha uchunguzi wa kile kilicho daiwa kwamba ardhi hiyo ilikuwa na madini masiku yakakatika, muingiliano Kati ya wakulima na wafugaji ukatokea na kusababisha vita kubwa Kati ya raia hao waliokuw wakiishi kwa nafasi na amani. Kwa utaratibu mwenyekiti mwenye macho ya utosini akaitisha mkutano ili kusuluhisha tatizo hilo la kutisha.

"Ndugu zangu naomba muwe watulivu, tumepata muwekezaji ambaye amekuja kuwekeza katika sekta ya kilimo kiwanda kitachukua kutoka kwenu malighafi tofauti tofauti zikiwemo ngozi, maziwa pamoja na mazao mbali mbali ya biashara hivyo mnaombwa kuwa watulivu kwani muda usiopungua wa miezi miwili mtakuwa mmeshalipwa fidia za kutosha". Akasema mzee Tumbotumbo kwa kauli za asali na kufanikiwa kutuliza hasira za wananchi hao. Kiwanda kikasimamishwa na mitaro mikubwa ya kutolea maji machafu ikajengwa na kuelikezewa kwenye maji.ardhi ikakauka na maji yaliyokuwa yakitumiwa na wananchi hao taratibu yakaanza kuua mifugo na kusababisha magonjwa ya matumbo kwa wananchi.

"Ziko wapi fidia zetu!! huyu kiongoz wa ardhi ya dhahabu amejichimbia wapi!! si yeye wala familia yake ni yenye kuiongelea hali hii tata!!".Aliuliza kiongozi wa wafugaji kisha kwa ghadhabu kubwa wakaandamana na kuelekea nyumbani kwa mwenyekiti. Ukimya ulitawala eneo lile huku sauti pekee iliyokuwa ikisikika ni ile ya mtoto mdogo wa mwenyekiti ambaye alikuw akilia.hodi ikapigwa na kwa haraka akatoka mke wa mwenyekiti akiwa na mtoto mkononi alupoulizwa kuhusu mumewe akadai kwamba mume wake aliamua kumtoroka baada ya kupokea pesa nyingi kutoka kwa muwekezaji.

"Anhaa...ng'ombe wetu wanakufa kila siku na wewe pamoja na mumeo mkulima mmeamua kutuibia kilicho chetu!!! Aliuliza kiongozi wa wafugaji na kuamuru binti yule akatwe katwe mapanga.

Mauaji hayo ya kikatili yakatekelezeka na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu. Taarifa zikawafikia wakulima na kwa hasira wakaamua kujikusanya na kuendeleza vita dhidi yao.harufu ya damu ikatapakaa na kumfikia simba wa nchi mwenye busara za farasi na hasira za mbwa mwitu akiandamana na wanahabari mpaka eneo husika na kukuta ardhi ya dhahabu ikiwa imetapakaa damu na udhalimu

" Uchu!! uchu!! uchu!! akasema kwa mkazo, matumbo yao yamejaa njaa.hawaridhiki wanapolishwa ila mpaka wale ziada, hawaakisi yaliyo ya kweli ila wafanyayo ni kwaajili ya choyo zao!!". anasema simba wa nchi, akiwalaani wale wote wanaopenda kuichafua taswira halisi.

" Hawakuwepo wakati moto ulipokuwa cheche, wakadharau na ule moshi uliotesa mifugo yetu, sasa yametokea simba wetu nani tumlaumu!".

" Zilaumuni nafsi zenu kwa pupa! bila kujali sheria mikononi mkaitweka! ni watendewa ila mengi mnayafanya tena yasiyo na maan na yenye kuangamiza umma!". kwa sauti akanguruma na kwa kuwageukia wafikwa

" Mwenye kutaka haki na afuate busara zangu, hakuna tabaka la wakulima wala wabeba virungu, tafuteni wawakilishi na sio mafisi, uzuri wa nchi yenu muuakisi wala msifuate ya wazushi na shida zao mkaziishi, kumbuka ni simba mmoja eneo zima aunguruma, anahitaji wawakilishi wenye hekima na tabia njema".

ujumbe huo uliwafikia wana kijiji, wakabaki wamejiinamia huku pua zao zikianza kuihisi harufu ya damu walizo mwaga. Kwa mikiki muwekezaji akashtakiwa na kupokonywa kiwanda ambapo kiwanda hiko kikaridishwa mikononi mwa serikali na matunda ya kiwanda hiko yakaanza kuonekana.upande wa mwenyekiti ambaye alikuwa amekimbilia mjini

ukiachana na serikali iliyokuwa ikimtafuta kwa udi na uvumba, taarifa za kuuliwa kwa aliyekuwa mpenzi na mama wa watoto wake zilimshtua sana kiasi cha kupandisha presha na kupoteza maisha huku akiziacha pesa ambazo alizitafuta kwa damu na moto zikichukuliwa na wenye nchi yao.

Ujumbe: wananchi wanatakiwa kuweka uzalendo mbele kabla ya chochote kwan yeyote kwa muda wowote anaweza kuwa kiongozi

Wananchi pia waache kuishi kwa matabaka kwani matabaka huvunja maelewano baina ya pande mbili au zaidi

Serikali ijitahidi kuchukua hatua za haraka na uhakika linapotokea tatizo kwani wahenga walisema usipoziba, ufa utajenga ukuta

Wananchi Tuache tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani kila nchi ina sheria na taratibu zake

Simba wa nchi akanguruma huku akianza kuondoka hatua moja ya mbele haikuzaa ya pili akageuka na kunguruma tena kwa nguvu zaidi ngruuuuu vichwa vya wananchi vilivyokua chini vikainuka kutazama na akanena kuwaambia"Hivyo mlivyo ndivyo muwe, wasikivu wenye kujutia makosa na muuishi upendo uungano na umoja na mkihisi tofauti mjifikilie kama mngeliungana juzi jana mngeliuana kiasi hiki? na je msingepata haki kwa kuwa wamoja?

Uzembe wa kuzishuhurisha akili, ukosefu wa uzalendo ukakifanya kijiji hiki kuludi nyuma kimaendeleo watu walipungua wazee wakazidi vijana waliishia vitani lakini hekima na uzalendo wa wazee waadithiaje wa hadithi Unategemewa kukuza vijana wapya wenye maalifa ya juu na uzalendo ....

Ukijani ukaonekana kijijini, furaha na shangwe zikashamiri,umoja na ushirikiano ukawa nguzo ,simba wa nchi si yule simba lakini ni yule simba wa nchi kwakufunzwa uzalendo.[emoji2772][emoji112][emoji113] Mwisho!!
 
Upvote 0
Back
Top Bottom