TanzActive
JF-Expert Member
- Nov 14, 2007
- 367
- 73
- Thread starter
-
- #41
Nilikuwa wa kwanza kituoni hapo na walipoitwa na msimazi wa kituo wakajitambulisha nilikuwepo na nilisikia mazungumzo yaouliwezaje kuwatambua wakati hawana ID za kimavazi au hao walikuwa nazo??
Anyway, mi nimeshapiga kura na nikiwa mle kituoni ukatokea utani fulani nikamsikia wakala mmoja akisema mwaka huu HADUNGANYIKI!!
na mm nikaungana nao kwenye tabasamu, baada ya hapo nikaenda pale kwenye kichumba nikamsalimu Dk wa ukweli na vijana wake nikakunja karatasi zangu na kuzitumbukiza sehemu stahili na tabasamu langu pana nikawapishe wengine nao watoe hukumu..
Roho inauma ukiibiwa huku unaona lol .
Nimefika Mapambano A Sinza, kuna tatizo la upungufu wa wasimamizi waelekezaji wa wapiga kura. Walibandika huko siku za nyuma list ya wapiga kura, leo wametoa pale yalipokuwa na kuyahamishia kwenye madarasa mbali mbali, lakini hakuna mtu wa kuelekeza wapiga kura hili jambo, hivyo watu wanafika na kusumbuka kutafuta majina yao, na wengine kukata tamaa, nimefanikiwa kujaribu kuelekeza watu kama kumi hivi, lakini sioni msimamizi wa kituo, askari na hao wasimamizi wa tume hawana usaidizi wowote wamekaa, kwa sasa watu ni wachache sijui itakuwaje pale kutakapokuwa na watu wengi.
Kama kuna mtu anamjua mtu wa tume anayeweza kusaidia hili ataarifiwe.
Acheni ujinga wenu mlikuwa wapi kufuatilia na kusaidia majimbo yasiyokuwa na mawakala leo uchaguzi umeanza ndiyo mnajifanya kutaka kusaidi, wezi wakubwa, Jimbo la Ubungo halina wakala hata mmoja haya basi nendeni mkasaidie.
Nimepitia threads kadhaa hapa na kugundua kuwa kuna baadhi ya members humu wamepiga kura tayari lakini humo ndani waliwakuta mawakala waliowatilia shaka kuwa si wa CHADEMA au hawakuwakuta kabisa. Sasa badala ya kuendelea kupoteza muda, ni vyema mwenye wasiwasi aweke jina la kituo hapa ili hatua zichukuliwe haraka kabla ya zoezi la kuhesabu kura halijaanza. Orodhesheni vituo hapa:
1.
2.
3.
.
.
.
n.
Ndugu zangu wana JF, suala la mawakala inaonekana linaweza kutia doa kwenye hatua hii ya mwisho ya kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa manyang'au. Inaonekana chadema hawakuweka sawa suala la mawakala. Maeneo mengi matokeo yanaweza kuchakachulikwa kwa sababu tu ya uzembe wa aina hii. Tafadhali viongozi wa chadema lifanyieni kazi suala hili (kama uwezekano huo upo) kabla halijaleta madhara. Taarifa tunazopata kutoka jimbo la nyamagana Mwanza siyo nzuri.
Inabidi chadema wajipange kuwaangalia hao mawakala kanjanja wa ccm
Utaratibu uliopo hata mawakala wasipokuwepo sio tatizo hata kidogo... kila karatasi inaandikwa aliyepiga ni card namba ngapi... hili nilikuwa lisijue.