APPROXIMATELY
JF-Expert Member
- Aug 10, 2021
- 2,035
- 2,715
Habari zenu wana JamiiForums..
Moja kwa moja naenda kwenye mada husika kama kichwa kinavyojieleza,kipindi nikiwa mdogo wa miaka 4 na kuendelea,nilikuwa na shangaa sana wazazi wanavyojianda kwa ajili ya christimass.
Wazazi walitununulia nguo kwa ajili ya christimass,nakumbuka baadhi ya nguo zilikuwa zinapendwa kipindi kile,kuna t-shirt na pensi ya njano yenye chata la kichwa la ngombe kwenye t-shirt (CHICAGO BULLS) yani ilikuwa nguo pendwa sana kipindi tukiwa watoto,kila mtoto alikuwa anayo, kipindi kile soda ilikuwa deal sana,nakumbuka baada ya kula li pilau la maana mama Alininunulia Fanta orange sio hizi za sasa hivi kipindi cha nyuma Fanta kweli ilipendwa sana na watoto,Pepsi hata ilikuwa haina soko.
Kipindi kile TV zilikuwa ndo zimeanza kutoka,baada ya kula pilau baba anatuwekea picha la yesu daah ilikuwa burudani sana,kweli maisha yanakimbio sana,hayarudi nyuma tena.
Saa 8 mchana tunaenda disco toto triple A,AU Tunaenda kukodisha baiskeli na kuenda uwanja wa soweto kuzunguka kwenye zile nyumba za kontazi,ilikua burudani maisha yalikuwa matamu sana,hapo mzazi kanipa buku la sikukuu.
Baada ya miaka kwenda mbele kidogo,ilipokuwa inakaribia christimass tarehe 23,24-25 tunaenda kukata mitarakwa ni miti ya christimass,alafu ilikuwa ina patikana kwa wingi line police arusha,yani ilikuwa hatari police walikuwa wakali sana hawakutaka miti yao ikatwe ovyo,mitarakwa yenyewe tulikuwa tunaiuza town.
Maisha yamekwenda kasi sana,majukumu kibao christimass kwangu sio deal tena,na baki kuwafurahisha watoto wangu kama nami walivyokuwa wananifurahisha nilipokuwa mdogo,nao zamu yao waenjoy maisha..
APPROXIMATELY..
NAKARIBISHA MJADALA..