Clinton Manangwa
JF-Expert Member
- Feb 1, 2017
- 214
- 223
Gram 1 ni shingapi kwa sasa
Kama huna ABC ya bihashara hii, nakushauri hiyo pesa nunulia watu pombe wanywe wakusifu. Hii bihashara ni zaidi ya uchawi.Mi natamani sana kuwekeza katika biashara hii lakini sijui maeneo gani yanaleta uhakika wa kutopoteza mtaji mf: kuwa na mwalo wa kusafisha dhahabu, kununua na kuozesha mchanga, ama kuchimba kabisa
Mi natamani sana kuwekeza katika biashara hii lakini sijui maeneo gani yanaleta uhakika wa kutopoteza mtaji mf: kuwa na mwalo wa kusafisha dhahabu, kununua na kuozesha mchanga, ama kuchimba kabisa
Hapo ulipo mwambia akuje PM, naona ndio umekosea mkuu.Mkuu wasikutishe eti uchawi unahusika hakuna vitu kama ivo nifuate PM nikujuze zaidi hata kuwekeza inawezekana maeneo ni mengi sana na karibu lakini jipange mtaji tu.
Hapo ulipo mwambia akuje PM, naona ndio umekosea mkuu.
Sababu kama kweli unayo nia njema na mhusika, haipo sababu ya kukimbilia PM kana kwamba kuna jambo la siri unalo taka kumueleza
Umeeleza vyema mkuu.Wakuu ngoja nifunguke hapahapa ili isijekuonekana kama mimi ni kanjanja aiseee kiukweli ili uweze kuwekeza katika uchimbaji mdogo kwa uzoefu wangu ni lazima usipungue mtaji wa Milioni thelasini 30,000,000/= halafu ukitaka kuozesha mchanga kama unaanza lazima uwe na Milioni miamoja 100,000,000/= hapo unakua umejenga plant humo humo ndani ya pesa hiyo na mtaji umebaki mkubwa wa kuanzia wakuu na napenda mnielewe siokwamba nilimwambia mtu mmoja anikute PM lakini nikataka kuonekana tapeli fulani wakuu.
Umeeleza vyema mkuu.
Ebu naomba unifanyie kunyumbua hiyo 30 milioni.
1. Je, unamaanisha hapo nitaanzisha duara (shimo), kulisha wachimbaji, kutoa vifusi pamoja na unyonyaji wa maji toka shimoni?
2. Je, kama ninahitaji kuozesha mchanga, kujenga processing plant kama ulivyo tangulia kusema.... je hii 100 milioni inatosha kusomba kifusi madini, kujenga jiko la uchomaji (refinery smelter), madawa ya kuchenjulia, umeme na maji, structures, malipo ya wafanyakazi na kadhalika?
Kwasasa naomba niishie hapa
Mkuu, kwa aelezo haya naomba nihitimishe kwa kusema kwamba umeanzisha mada ngumu ilio kuzidi kimo.Aaaaah mkuu hii milioni 30,000,000/= nikweli unaweza kuchimba duara vizuri lakini kwenye maji itaongezeka na nimemaanisha maeneo ambayo hayana maji na ukifika kwenye maji tayari utakua umeshazalisha na utakua na nguvu hata ukianza kuvuta maji utaongeza kidogo tu halafu kuhusu plant nimemaanisha ni kujenga tu tena tank 6 na hela inayobaki utaanzia kanunua maozesho na madawa ya kuanzia lakini angalizo hiyo ghalama ni kibongo bongo kulingana na mitaji yetu na kuhusu jiko tena standard lazima uwe 1bilion mkuu.
Mkuu hebu jaribu kuchangia unachokijua ,usijaribu kucrush mwenzio,yeye amejaribu kutoa yake ...kama unajua zaidi na wewe changiaMkuu, kwa aelezo haya naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Umeanzisha mada ngumu ilio kuzidi kimo.
Wewe unacho kijua ni kuhusu wachimbaji na hakuna unacho kijua kuhusu biashara ya uchumbaji...
Hivi kati ya kuwa mchimbaji na mnunuzi wa dhahabu ni bora kufanya kipi?
SadiMkuu wasikutishe eti uchawi unahusika hakuna vitu kama ivo nifuate PM nikujuze zaidi hata kuwekeza inawezekana maeneo ni mengi sana na karibu lakini jipange mtaji tu.
Asante kiongozi.Mkuu kwa kawaida wote wanaitwa wachimbaji lakini inategemeana ila walio wengi walianza kuwekeza katika kuchimba halafu wakapanua wigo katika ununuzi na pia ili uweze kuwa mnunuzi mzuri anayeweza kuepuka hasara nyingi ni bora ukaanza kuchimba ili uzifahamu changamoto maana ni nyingi sana mkuu.