Miaka hio,kuna jamaa alienda wanapouza mkaa kwenye magunia,yale makubwa kipindi hicho. Akambebesha lile gunia akamwambia twende pesa ipo nyumbani, wametembea wakafika sehemu kuna hardware, jamaa akamwambia muuza mkaa kama una pesa hapo nipe ninunue cement walete home, hela ya mkaa na hii nakupa home,jamaa akatoa mauzo yote, safari ikaendelea.
Sasa sisi asub hio niko bro na Mzee, tunakuta mtu mmoja anatua mkaa njee,mwingine kaingia,akaanza uliza kuna vyumba vya kupanga hapa,tukamjibu hatupangishi ila kuna jirani hapa kaangalie,tunatoka tunamwonesha hio nyumba, yule wa mkaa kakalia tu gunia. Yule jamaa akaenda akaongea kidogo na yule wa mkaa akawa anaondoka.
Kama lisaa mbele tunakuta wa Mkaa anagonga getini anauliza mbona kaka yenu harudi na mkaa amwingizi ndani. Kumbe jamaa alimwambia pale ni kwao na Muda ule tumetoka tunamwelekeza nyumba ya jirani, ndio ule Muda akamfuata jamaa akamwambia baba ananituma nyumba ile,maana wakatianamwelekeza alikua anainyoshea kidole