Kyambamasimbi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 762
- 1,597
Habari ndugu wajf. Kwa ujumla maisha Yana ladha na mitindo tofautitofauti, hapa kwetu uswahili panaitwa mji mpya Kichangani Manispaa ya Morogoro, Pana maisha ya kipekee Sana ukiachilia mbali mitaa kama Chamwino. Mida kama hi unakuta ndio watu wanawasha majiko kwaajili ya kuchomea kuku broiler na chipsi za jerojero, pia unakuta na wamama mida kama hii ya usiku hadi wadada wametoa majamvi wako vibarazani wanapiga zogo sijui wanapika saa ngapi, Cha ajabu unakutana na watoto wadogo wako mitaani wanacheza.
Halafu wezi na vibaka wanafahamika akikwapua anakimbilia nyumba yoyote ukiuliza na ukakutana na mbibi atakwambia kapita kumbe yupo ndani kamficha akitoka anampa mbibi 1000 imeisha hiyo . Maisha haya. Acha tuu. Kwenu kukoje?