muendelezo,
Baada ya kukubali kusafiri nae,safari ilikuwa usiku tofauti na vile ambavyo nilitarajia huku tukitumia gari binafsi la wafanya biashara wa kikongo man,Asubuhi tulikuwa tunamalizia shughuli za pale uhamiaji kwa ajili ya kuingia congo.Safari iliendelea vizuri huku nikionyeshwa maeneo mbali mbali na wenyeji wangu huku nikipewa stori za hapa na pale.
Mwendo wa masaa 4,tukakuta kuna wanajeshi walivyoona tu gari yetu wakarusha nywaya barabarani,nilishtuka sana lakini wenzangu hakuna walio stuka wakanishusha uoga na kunambia kuwa askari wa congo ni tofauti na wa tanzania kwani wao huwa hawasimamishi gari na mkono bali ni kuweka vizuizi bara barani au hata kupiga risasi,na hata ndipo ninapoweza kuthubutu kwa kusema kuwa congo ndo inaongoza kwa rushwa kwani tulitoa rushwa ya dola 200,machoni mwa watu tena bila uoga.Tulikuwa tunaenda kijiji cha kalupash ambacho ni mwendo wa masaa 5 baada ya kuvuka msitu wa goma.Tulianza kuukata msitu wa goma saa 12,asubuhi hakika ulikuwa ni msitu ambao sijawahi kuuona katika maisha yangu.Baada tu ya kuuanza msitu kila mtu akajikuta tu amekuwa kimya pasipokuongea lolote.
MATATIZO YANAANZA
Tukiwa ndani ya msitu baada ya nusu saa tuona kama gogo limelazwa barabarani kwa mbali baada ya kusogea vizuri tukaja kugundua kuwa walikuwa ni watoto wawili ambao walikuwa wamelala barabarani huku wakiwa na bunduki kutuelekezea sisi,alafu kwa nyuma yao kulikuwa na wengine wamewashikia wenzao mkanda wa risasi ambao ulikuwa umeunganishwa kwenye bunduki zao.Dereva baada ya kuwaona akatuambia sasa ba mutu muswali buswala ma mwisho.Hakuna aliyeuliza alimaanisha nini lakini kwa kilichokuwa mbele yetu ote tukawa tumeshaelewa lakini cha ajabu hakuna aliyeswali zaidi ya kuanza kulia.Tulivyowakaribia tu walipiga risasi kama 20 juu wakitutaka tushyke ndani ya gari huku na wengine wakubwa wakiwa wanatoka msituni.Walikuwa ni warefu na wenye miili mieusi ya kutisha mno ambao kimuonekano tu walikuwa wanawakilisha kifo katika maisha basi ote tukashuka kisha mmoja akaingia kwenye gari na kushusha kila kitu.
Baada ya hapo kila mmoja wetu akawa anaitwa mbele na kuuljzwa maswali kwa kilingala kisha anawekwa pembeni,kiupande wangu sikuwa naelewa chochote,ilipofika zamu yangu nilikuwa natetemeka mno kiasi cha mikojo kutaka kunitoka nikaskia wakitaja tanzania kisha wenzao wakawa wanaitikia,kuskia hvyo nikamwambia yule jamaa nisamehe mdogo wangu dah,baada ya kusema hvyo nilipigwa na kitako cha bunduki cha kwenye tumbo kidogo nijinyee kama siyo kuzimia[emoji17][emoji17][emoji17].Kumbe ni kosa kubwa kumuita mtoto au mdogo,askari au muasi yeyote wa congo,baada ya hapo tukaamriwa ote tuvue nguo tulizovaa,tukatii amri ote kwenye costa tukavua ngua hakika tulikuwa tunalia kama watoto wadogo,kisha tukaachwa tuendelee huku tukiwa uchi vile vile baada ya wazee tuliokuwa nao kuwatia huruma,Tuliondoka mbio na gari yetu hali ya kuwa tukiwa uchi wa mnyama huku nafsi yangu ikiwa inajuta mno kwanini nilikubali kwenda
NITAREJEA KUMALIZIA