UZI MAALUM.kwa wale tulotoka mikoani Kuja dar

UZI MAALUM.kwa wale tulotoka mikoani Kuja dar

madindigwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2017
Posts
2,488
Reaction score
2,904
Nakumbuka ilikua mwaka 2004 tarehe 16 mwezi 4 ndio nilikua new arrived.katika hili jiji lenye kila Aina ya mambo, siku ya tarehe ya safari ukweli sikulala hata kidogo Kwa hofu ya kuchelewa usafiri.nililala usingizi wa mag'amug'amu na ndoto fupi fupi hasa kuhusu jiji dar ambalo binafsi nilikua naliona kupitia taarifa za habari au tamthilia kama mambo hayo za Akina bishanga bashaija kipemba bamboo na wengineo wengi.

Hauchi umekucha mapema na alfajir nafikir ni Kawa mtu wa kwanza kufika kwenye basi.tuakanza safari mungu si athuman nafikir tulilala moro.kulipo kucha ndipo tukaanza safar na saa nne tushafika dar.
Kitu cha kwanza kilicho niogofya ni Hali ya joto kuu ambalo sikuwahi kulipata tangu kuzaliwa kwangu huko maeneo ya geita, dar nikawaza Mungu wangu ntaweza Hali hii basi akaja mwenyeji wangu na kunichukua mpaka maeneo ya I lala huko ndio nilipo Anzia maishaa.maisha yalikua magumu sana hata nikajifikiria kurudi home

Niliwamic marafiki ndugu na jamaa hata nilikata shauri nirejee tu nyumbani Kwa upande wa chakula ulikua taabu saana kwangu ugali kama uji tena kadogooo ukweli hiyo Hali ilinisumbua saana, hasa ukizingatia sisi tushazoeaa ugali mgumu mkubwa mboga za kukomba we acha tu.

Hapo ndipo nikakumbuka kauli tulizo kua tunaambiwa watu wa dar ni wachoyo,
Geto tulokua tunakaa dirisha moja watu kibao mvua ikinyesha linavuja kinyamaa.ukweli Dar ilikua kama jehannam kwangu siwezi sahau.siku miezi mwaka miaka imepita ni uvumilivu tu Leo ukinipeleka mkoani ntakwenda kufanya kazi gani, wakati sasa mji uko mikononi wangu, nimepata ndugu jamaa marafiki mambo yanakwenda japo Kwa mwendo wa mbuzi mbele kamba nyuma kiboko.

Dar ukilemaa huwezi hata kukumbuka kurudi kisalimia nambie ww wa mkoani ulikujaje kwenye jiji hili.
 
Daa watu mna misemo atii mbele kamba nyuma viboko.
Hakuna jinsi mtaaluma pambana tu wanaume tumeumbwa Mateso
 
Huwezi kuwaona hapa...ndio hao hao kila mara utawasikia wanabana pua 'wanaume wa Dar...'
 
Back
Top Bottom