Uzi Maalum: Tetesi za soka Ulaya 2017

TETESI ZA USAJILI TAREHE 17.07.2017
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda bado akahamia Liverpool kwa pauni milioni 60 msimu huu. Mchezaji huyo amesisitiza anataka tu kwenda Liverpool. (Sun)


Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 45 kumtaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Express)


Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amepigwa picha kwenye Instagram akiwa amevaa jezi ya Atletico Marid na kuandika "mpe salaam zangu Conte". (Mail)


Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku, 24. (Sky)





Chelsea wameonywa na Borussia Dortmund kuwa wana wiki moja tu ya kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang. (The Sun)




Aubameyang alijiunga na Borussia Dortmund kutoka St Etienne in 2014
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anadhani kuwa ataweza kumshawishi Alexis Sanchez, kutoondoka Emirates. (Mirror)




Vinginevyo Arsene Wenger anafikikia kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele, 20. (Star)




Arsene Wenger amekata tama ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, na badala yake sasa anaelekeza nguvu katika kumsajili Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Telegraph)





Arsenal pia wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, kuziba nafasi ya Alexis Sanchez ikiwa ataondoka. (Don Balon)





Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya Monaco kumuuza kwenda Arsenal. (Sun)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anakaribia kuhamia Juventus kwa pauni milioni 8. (Daily Mirror)




Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Star)





Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitano winga wa Atletico Madrid Yannick Carasco, 23. (Don Balon)



Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka Toni Kroos, 27, kuwa sehemu ya mkataba wowote utakaomhusisha David de Gea kwenda Real Madrid. (Sun)



Manchester United wanaonekana kukaribia kumpata kiungo wa Inter Milan Ivan Perisic. (Daily Mirror)



Zlatan Ibrahimovic amekataa nafasi ya kujiunga na LA Galaxy na anapanga kusaini mkataba mpya na Manchester United. (The Sun)





Paris Saint-Germain wanapanga kutoa euro milioni 150 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio. (Don Balon)



AC Milan wananamnyatia mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Gazzetta dello Sport)





Barcelona wapo tayari kutoa euro milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumsajili Marco Verratti kutoka PSG. Calciomercato)


Tottenham wanataka kujaribu tena kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. Timu hizo mbili zimeshindwa kukubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. (Independent)



Tottenham wana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19, mwishoni mwa wiki hii. (Mirror)





Loic Remy, 30, anatazamiwa kuondoka Chelsea msimu huu, huku Everton na Southampton zikimtaka. (Metro)





West Ham watapanda dau la tatu kumtaka winga wa Stoke Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la awali kukataliwa. (Sky Sports)





Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 18.07.2017



Mabingwa wa England, Chelsea wana “nia thabiti” ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Sky Sport)



Chelsea wanazungumza na Manchester City kuhusiana na usajili wa Sergio Aguero. (beIN Sporst)



Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic hayuko tayari kulipa fedha nyingi kumsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo anaelekea Italia. (Star)




Chelsea wanafikiria kumrejesha tena Stamford Bridge, beki wa Southampton Ryan Bertrand. (Evening Standard)





Chelsea wanataka kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang. (Sky Sports)



Dau la pauni milioni 2.6 la Manchester City kumtaka kipa wa Napoli, Pepe Reina, 34, limekataliwa. (Mirror)




Manchester City hawatakabiliwa na ushindani tena kutoka Bayern Munich katika kumsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge kusema hawamfuatilii tena. (Manchester Evening News)





Paris Saint-Germain wameingia katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis sanchez, 28. (Daily Mirror)




Paris Saint-Germain wapo tayari “kuvunja benki” kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Neymar, na watakuwa tayari hata kulipa euro milioni 222, kulazimisha uhamisho wake. ( GianlucaDiMarzio.com )




Washauri wa karibu wa Neymar wanamshauri aondoke Barcelona ili kuepuka kufunikwa na Lionel Messi. Manchester City, PSG na Manchester United zote zinamtaka mshambuliaji huyo kutoka Brazil. (Sport)





Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona amesema hakuna timu itakuwa tayari kutoa pauni milioni 195 kumsajili Neymar, 25. (Mail)




Manchester United wanafikiria kupanda dau la mwisho la pauni milioni 60 kumtaka kiungo wa Tottenham, Eric Dier, 23. (Mirror)





Zlatan Ibrahimovic, 35, ameonesha dalili kuwa atabakia Old Trafford baada na kuwaandikisha watoto wake katika akademi ya Manchester United. (Sun)




Manchester United wanamtaka kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huku klabu yake RB Leipzig ikipunguza vikwazo. Mbali na United na Liverpool, pia Arsenal, Manchester City, Juventus na Inter Milan zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea. (Football Whispers)




Manchester United wana uhakika wa kukamilisha usajili wa Ivan Perisic katika saa 48 zijazo. (Starsport)




West Brom wanamtaka beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, lakini timu hizo mbili hazijafikia makubaliano yoyote. (Birmingham Mail)





Arsenal watajaribu kupunguza idadi kubwa ya wachezaji wake wasiotumika, kabla ya kufanya uamuzi wa kuvunja rekodi tena ya usajili na kumchukua Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Mail)






Monaco wamewaambia Arsenal watalazimika kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa takriban pauni milioni 80 kumsajili kiungo Thomas Lemar, 21. (The Mirror)




Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 6.2 kutoka Sampdoria la kutaka kumsajili kiungo Jack Wilshere, 25. Arsenal wanataka pauni milioni 8.8. (DI Marzio)
Juventus wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumsajili Nemanja Matic, 28, au Steven N’Zonzi, au William Carvalho. (Calciomercato)






Inter Milan wanapanga kuwajaribu Real Madrid kwa kutoa dau kubwa kumtaka kiungo Toni Kroos. (Sport Mediaset)




Crystal Palace wanakaribia kumsajili beki wa Ajax, Jairo Riedewald, 20 kwa pauni milioni 8. (Evening Standard)




Crystal Palace wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumchukua Jack Wilshere kutoka Arsenal kwa mkopo. (The Sun)





Crystal Palace wapo tayari kutoa pauni milioni 16 kumsajili beki wa Arsenal Callum Chambers, 22. (Telegraph)




Beki wa kushoto wa Nice ya Ufaransa Dalbert Henrique, 23, amethibitisha kuwa Liverpool wanamtaka, lakini amesema dau kutoka Inter Milan ni la kuvutia zaidi. (Express)





Riyad Mahrez, 26, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aweze kujiunga na Roma. (Leicester Mercury)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 27, anakaribia kujiunga na Juventus. (Guardian)




Winga wa Hull City, Ahmed Elmohamady, 29, anakaribia kujiunga na Aston Villa. (Hull Daily Mail)




Beki wa kushoto wa Hull City Andy Robertson, 23, anakaribia kujiunga na Liverpool kwa pauni milioni 8. (Liverpool Echo)




Mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, 28, hajasafiri na kikosi kilichokwenda Marekani na huenda akarejea tena Swansea. (Wales Online)




Beki Matheiu Debuchy wa Arsenal anatarajiwa kujiunga na Nice ndani ya saa 48 zijazo, baada ya kushindwa kuwika Emirates. (Europe1 Sports)





Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 19.07.2017




Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali dau la Paris Saint-Germain, baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kuwa tayari kutoa pauni milioni 195. (Esporte)




Makamu wa rais wa Barcelona Jordi Mestre amesisitiza kuwa Neymar hatoondoka Barcelona wakati wowote ule. (Star)





Mtaalam wa soka wa Amerika ya kusini Tim Vickery amesema Neymar huenda akaondoka Barcelona ili kuepuka kuwa chini ya kivuli cha Lionel Messi. (BBC Radio 5 Live)




Kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, anataka mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki ili kujiunga na Tottenham, huku klabu yake ya Everton ikitaka pauni milioni 50 kama ada ya uhamisho. (Mirror)




Tottenham watalazimika kumlipa kiungo Moussa Sissoko, 27, ili aondoke, licha ya kutoa pauni milioni 30 kumsajili mwaka jana tu. (Daily Mail)




Arsenal watajaribu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzima, 29, iwapo Alexis Sanchez, 28, ataondoka Emirates. (Don Balon)




Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema Alexis Sanchez, 28, anayesakwa na Manchester City, hauzwi. (Sky Sports)




Paris Saint-Germain wameibuka tena na lengo la kumtaka Alexis Sanchez, 28, na wana uwezekano mkubwa wa kumsajili. (Telegraph)





Wakala wa Alexis Sanchez amewapa Real Madrid nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa Arsenal, lakini Real wamekataa kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona. (OK Diario)





Newcastle na Crystal Palace wanafikiria kumchukua kipa wa West Ham Adrian, baada ya klabu yake kumsajili kwa mkopo Joe Hart kutoka Manchester City. (Mirror)




Swansea wamemuulizia mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, 28, aliyecheza kwa mkopo Stoke msimu uliopita. (Foot Mercato)




Ivan Perisic, 28, amesafiri na klabu yake kwenda China baada ya Manchester United kushindwa kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho na Inter Milan. (Telegraph)




Manchester United wameacha kumfuatilia kiungo Eric Dier, 23,wa Tottenham baada ya klabu hiyo ya kaskazini mwa London kukataa kumuuza mchezaji huyo. (Mirror)



Manchester United wamekuwa na mazungumzo ya awali na Paris Saint-Germain kuhusu kutaka kumsajili Marco Verratti. United wapo tayari kupambana na Barcelona kutaka kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Italy. (TuttoMercatoWeb)





Borussia Dortmund wameamua kutomuuza Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na kuhamia Chelsea kwa pauni milioni 70. (Kicker)




Chelsea hawataki kutoa euro milioni 30.8 wanazotaka Real Madrid kwa ajili ya beki wa kulia Danilo. (Evening Standard)





Beki wa Southampton Virgil van Dijk hajawasilisha maombi ya kuondoka kama njia ya kulazimisha uhamisho wake kwenda Liverpool. (Daily Echo)




Beki wa Barcelona Aleix Vidal amekataa nafasi ya kuhamia Juventus, kuziba pengo la Dani Alves aliyekwenda PSG. (Sport)





Arsenal wanakaribia kumsajili mshambuliaji kutoka Feyenoord Joshua Zirkzee, 16, aliyekuwa akinyatiwa na Ajax. (SoccerNews)





Jack Wilshere, 25, ameambiwa anaweza kuondoka Arsenal. (Mirror)




Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa psg mwisho wa,sku watakosa yote sio neyma wala,Sanchez wapunguze tu jazba walio nayo

Nataman arsenal tungemchua
Huyu jamaa wa Dortmund pamoja na morrata lakib ndyo
Hvyo,n ndoto tu za mchana

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Hiv rashford hauwz,hakuna
Hata club moja iyojitokeza
Japo kwa utan tuu

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 20.07.2017
Paris Saint-Germain wanajiandaa kuzungumza na Barcelona kuhusu uhamisho wa pauni milioni 196 wa Neymar, 25. (Guardian)
PSG wapo tayari kumpa Neymar pauni milioni 45, za kukubali tu kujiunga nao, na mshahara wa pauni 596,000 kwa wiki (baada ya makato ya kodi) na mkataba wa miaka mitano. (Daily Mail)
Barcelona wanapanga kuzungumza na Monaco kuhusu kumsajili Kylian Mbappe, 18. Barca wanatarajia kupata fedha za kutosha kumsajili Mbappe baada ya kumuuza Neymar, 25. (Daily Mail)
Chelsea wanataka pauni milioni 44 kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Diego Costa, 28, baada ya kukamilisha usajili wa Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid. (Independent)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema hakuna uhakika thabiti iwapo Diego Costa atakwenda Atletico Madrid. (Mirror)
Chelsea, Tottenham na Manchester United huenda zikaingia katika mapambano ya kumgombania kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. (The Times)
Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, baada ya dau la pauni milioni 66 kukataliwa. (Mirror)
West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier ‘Chicharito’ Hernandez, 29, kutoka Bayer Leverkusen. (Sky Sports)
Arsenal wamewaambia West Ham kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 20 ikiwa wanamtaka kiungo Jack Wilshere, 25. (Daily Star)
Paris Saint-Germain wamemtuma mkurugenzi wao wa michezo kwenda London kujaribu kumshawishi Alexis Sanchez, 28, ambaye pia anasakwa na Manchester City. (Sun)
Everton wamepata matumaini zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30. (The Telegraph)
Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny amekataa kuhamia Leicester City waliokuwa tayari kutoa pauni milioni 10 kumsajili. (The Sun)
Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Danilo, 26, kwa pauni milioni 26.5. (Guardian)
Manchester city wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Benjamin Mendy, 23, kutoka Monaco. (Times)
Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti, 24, baada ya mchezaji huyo kumfanya Mino Raiola kuwa wakala wake mpya. (Sun)
Manchester United na Chelsea zilitazama uwezekano wa kumsajili Neymar, lakini timu hizo mbili zilikatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 196 ya mchezaji huyo, 25, kutoka Brazil. (Independent)
Inter Milan wamewaambia Manchester United lazima wamjumuishe Anthony Martial, 21, katika mkataba wowote utakaohusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28. (Independent)
AC Milan wamesema kiungo mshambuliaji wao Suso, 23, anayenyatiwa na Tottenham, hauzwi. (Tuttomercato)
PSG watamuuza kiungo Blaise Matuidi, 30, iwapo dau zuri litatolewa. (L’Equipe)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…