Uzi maalum wa chemsha bongo -brain teaser

Taxi driver amevunja sheria katka KEEP LEFT
badala ya Kupita LEFT akapita KULIA
Na trafik alikua hapo hapo kwenye hio round about,cha ajabu huyo trafik hakumsimamisha huyo Dereva wa taxi baada ya kumuona na anapita kulia badala ya kukeep left
Swali,, Je ni kwanini huyo trafik hakumsimamisha?
Ataepata jibu zawadi yake nono PM

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Huyo dereva taxi alikua anatembea kwa miguu, hakuwa anaendesha gari(taxi) yake.

Halafu taxi yake alishaniuzia toka mwaka jana, nashangaa bado anajiita dereva taxi.
 
Kipofu aliyekutwa na hatia, na kuhukumiwa kunyongwa, alipewa nafasi ya kuepuka adhabu hiyo kwa kupewa chemsha bongo:

Alikabidhiwa vidonge vinne vya rangi, viwili vyeupe na vingine viwili vyekundu. Vidonge hivi ni vya sumu lakini vikinywewa kwa viwango sawa vinashambuliana vyenyewe na havileti madhara, yani mtu akinywa kidonge kimoja chekundu na kimoja cheupe basi hatarudhika. Lakini akinywa vya rangi moja tu lazima afe.

Kipofu huyu aliambiwa ni lazima anywe vidonge viwili, akifanikiwa bila kudhurika basi ataachiwa huru.

Je, huyu kipofu atakunywaje hivi vidonge ili asalimike..?
 
vyote vinne anywe
 
sababu ni round about
 
Traffic hawakai round about

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipofu huyu aliambiwa ni lazima anywe vidonge viwili, akifanikiwa bila kudhurika basi ataachiwa huru.

Je, huyu kipofu atakunywaje hivi vidonge ili asalimike..?
Atavunja kila kidonge katikati na kunywa nusu moja, nusu nyingine ataweka pembeni.

Jumla atakua amekunywa nusu nne, ambazo ni sawa na kidonge kimoja cheupe na kimoja chekundu. Hivyo ataachiwa huru.
 
A boy is walking down the road with a doctor. While the boy is the doctor’s son, the doctor is not the boy’s father. Then who is the doctor?
 
Haya mkuu,unajua sana kuchunguza aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…