Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,824
- 2,264
Habari zenu wana JF,
Ni wazi kwamba watu wengi hatuna elimu ya kutosha jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa wapendwa wetu pindi wanapopata matatizo mbali mbali ya kiafya kabla ya kuwapeleka hospitali. Wakati mwingine mtu anaweza kupata tatizo litakalomfanya aweze kudumu kwa dakika chache tu bila kupata huduma ya kwanza.
Hali hiyo imepelekea watu kupoteza maisha wakiwa njiani kupelekwa hospitali au kupata ulemavu wa kudumu pengine kutokana na namna ya ubebaji au ukaaji akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Hivyo basi nawakaribisha watu (wataalamu) mbali mbali wanaojua jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa matatizo mbali mbali kama:-
Endapo mtu kapigwa shoti ya umeme unachotakiwa kufanya cha kwanza ni kuzima chanzo cha umeme kama kipo karibu na kinafikika kwa urahisi, hapa nazungumzia main switch. Kama chanzo kipo mbali au hakifikiki kwa urahisi unachotakiwa kufanya ni kumtoa muhanga kwenye eneo tukio ili asiendelee kupata madhara kwa kutumia kitu kikavu kisichopitisha umeme kwa mfano mti mkavu. Kamwe usimshike kwa mikono (bare hands) kwani na wewe kuna uwezekano ukapigwa shoti kupitia mwili wake. Mcheki kama anapumua kawaida na kama anashindwa msaidie kwa kumlaza chali huku wewe ukiwa umepiga magoti na kumkandamiza na kuachia (kama mtu anavyohema) kifuani kwa viganja vyako (tizama kiambatanisho). Kama bado hawezi kupumua, njia nyingine ambayo si salama sana kiafya hasa kipindi hiki cha UVIKO19 ni hii. Mpanue mdomo huku ukimziba pua, weka mdomo wako kwenye mdomo wake na kumpulizia pumzi (mouth to mouth inhalation). Kisha endelea kumgandamiza kifua na kuachia mpaka pale atakapoanza kupumua. Baada ya hapo mpeleke hospitali kwa matibabu zaidi.
Karibuni.

- Kuzimia.
- kuanguka ghafla kutokana na maradhi mbalimbali mf. presha, kisukari nk.
- kuumwa na nyoka
- kupigwa shoti ya umeme
- kupata jeraha linalota damu nyingi
- kuungua moto
- kushindwa kupumua
- kupata ajali
- kupaliwa/kwikwi mfululizo
- kukwamwa na kitu katika njia ya hewa au chakula (mf. mtoto kumeze sarafu au kisoda)
- kunywa sumu au chochote kisichofaa (mf. mtoto kunywa dawa kimakosa au mafuta ya taa)
- kuingiwa na sumu au chochote kisichofaa machoni.
- kuzama kwenye maji ya kina kirefu na kunywa maji mengi.
- kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisipokuwa/kikiwa bado ndani ya mwili wako
- Shambulio la moyo
- Kutapika/kuharisha mfululizo
- .....
- ......
- ......
- .......