Uzi maalum wa kujikumbusha mtaa wako uliokulia. Wa Majengo, Arusha tukutane hapa

Kuanzia Kona Ilboru hadi mitaa ya Kisiwani ilikuwa balaa... ubabe mwingi. Hiyo mitaa ilikuwa na wanariadha wengi
 
Ilkiurei ukipandisha kule juu Ngateu, ukishuka huku chini unakutana na white rose bar,kabla hujafika white rose hapa MANGURUENI mitaaa niliyotumwa sana maziwa.

Rudi huku mitaa ya kiranyi cheza sana mpira, njoo tupande kule juu ilboru tukacheze mechi ya kirafiki usiku turudi tuchokoze mbwa wa wazungu watubwakie tukimbie.

Serereka huku mianzini zurura sana, basi shule zitakua zimefunguliwa Niende zangu sanawari nipandishe kule Enaboishu class natulia zangu tuliii, usiku nitoroke nishuke hapa chini bishop durning tule tule romance na vitoto vya pale.

ki ufupi utotoni nili enjoy sana ila siku enjoy kivileee maana home saa 12 ndani ukichelewa ujue stiki zinakuhusu,sijawahi maliza wiki sijala stiki.

Arusha is my home,acha kidogo niende matejoo kununua njiwa kwa mwanangu Rasiiii,nimemkosa naingia pale magorofani nabeba njiwa wangu haoo hadi home.

nikiwa njiani napita technical pale nachuma majani ya sungura wangu,nanunua chuchuba tunatembea na chuchuba zetu huku mkononi nina majaniyangu ya sungura na njiwa wangu cheupeee na oraaaa hapa naenda toa mbegu kali sanaa.

Sema nini wanangu nimemiss primary,watoto wa levooo mnanijua eeeh nishasahau kubeba kidumu na mbolea,achana na mitoto ya TRUST inajitia ya kishua sema nimeshakua mkubwa mwanangu aende braeburn sasa,mateso yaliishia kwa baba ake.

Chugastani a.k.a United State
 
Aisee man unanifikirisha sana long
Kona Ilboru nilikuwa na marafiki wengi... kuna jamaa jirani na kina Kei alikuwa fundi simu, redio na electronics devices zingine. Na kuna mzee kada wa CCM muuza magazeti alikuwa mzinguzi kinyama.... Nilikuwa napenda kwenda kwa Mama Peruu jirani na Riadha Lodge kula kitimoto
 
Oya control mbona wewe wa nyumbani,ulikaaga mtaa gani
 
Unawajua kaka zake na molleli,
 
Hahaaa, Morogoro hiyo. Ilikuwa mitaa yangu ya kujidai hiyo.
 
Bongonyoo,jamuhuri,Kwa Ally Nyanya,mtaa wa jaluo[emoji16][emoji39][emoji16]Nairobishine bar...
 
Mkuu kahumba ulikuwa unaenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…