Uzi maalum wa kuombana msamaha, kupongezana na kutoa ushauri (2017 kwenda 2018)

Uzi maalum wa kuombana msamaha, kupongezana na kutoa ushauri (2017 kwenda 2018)

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Nimejaribu kutafakari nimeona toka January 2017 mpaka December 2017 ilikuwa safari ndefu yenye milima na mabonde mengi ambayo kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine amepitia.

Sasa kwa uzi huu malaamu basi ni wakati wa kila mmoja kutoa lake la moyoni kabisa kwa kuombana msamaha ila tuanze mwaka vizuri wa sisi na wengine nani ya JF bila kusahau kupongezana kwa mazuri tuliyofanya ndani ya JF na ushauri pia katika familia yetu hii kubwa ya zaidi ya wajumbe nusu milioni.

Upande wangu namshukuru Mungu kwa wote tuliochangia mada mbalimbali ndani ya JF kweli tumeelewa mengi tusioyajua na hata kufika mahali lugha zilikuwa kali lakini ni kweli hisia zilikuwa kali sana hasa pale Tundu Lissu alipopigwa risasi zaidi ya 30 nakumbuka JF ili trnd sana kwa taarifa zake na nilijaribu sana kuondoa dhana ya Serikali kuwa ndiyo ilihusika kumshambulia Tundu Lissu Mbunge wa Singida Magharibi...Nakumbuka sana nilipata upinzani mkali sana toka kwa watu mbalimbali lakini huo ulibaki kuwa msimamo wangu mpaka dakika ya mwisho.

Naomba MSAMAHA kwa wale wote niliowakwaza namna moja au nyingine katika mada zile lakini sikuwa na namna nyingine ni katika kuhakikisha tunapata ushahidi wa kutosha kuitia Serikali hatia ndipo maneno yale yawe na ukweli na si vinginevyo.

Nawapongeza wote waliotoa mada mbalimbali hasa za kuelimisha umma kuhusu afya,uchumi demokrasia,usalama,hali ya haki za binadamu,elimu n.k zimekuwa msaada tu.

Nataratijia mwaka 2018 utakuwa ni mwaka wa changamoto kubwa ktk vyombo vingi vya habari maana wengi sasa wanaanza kurudi nyuma kuandika mada kali,ukweli,na hasa hasa kuhusu namna ya kuishauri Serikali kwasababu tu ya wachache walioitwa na vyombo vya dola kuhojiwa kuhusu matamko yao au uhandishi wao.

Lakini ushauri wangu kwako tujitahidi kwenda na move ya Rais na kuangalia Taifa linataka nini kwa sasa inaweza kutusaidia kuwa huru kuandika mambo ya muhimu kwa mwaka 2018 bila kupata misukosuko.

Na hii hali ya kupinga kila jambo linalofanywa na Rais Magufuli mimi sijui limetoka wapi na nia yake ni nini kiukweli na ndilo linatoa hata maamuzi mengine yawe magumu kwasababu hujui kwanini hata ukifanya jambo zuri mtu ajitokeze apinge ...hebu TUJITAFAKARI HAPO...

HERIA MWAKA MPYA 2018 KWA KILA MWANA JF....KARIBUNI SANA
 
Mimi nawaomba msamaha watu wote wa jf kwa story zangu za kipuuz zisizokuwa na kichwa wala miguu, mwaka huu nastafu kurusha mastory ya kijinga

LONDON BOY
 
Mimi nawaomba msamaha watu wote wa jf kwa story zangu za kipuuz zisizokuwa na kichwa wala miguu, mwaka huu nastafu kurusha mastory ya kijinga

LONDON BOY
Beira Baby Boy safi sana na hongera sana na ubarikiwe tu kwa mwanzo mzuri huo katika kuhabarisha umma
 
hivi Rais akiomba toba ndiyo mambo yanabadilika au inakuwaje...maana hata sijawealewa wale wanaounga mkono kauli ya Askofu Kakobe?
 
kwanza wewe mwenyewe tramadol uanze kumuomba msamaha wa dhati kabisa TUNDU LISSU NA WANAJF WOTE WENYE MAPENZI NA TL !ulikua unatoa mada 4 kwa kila siku kumhusu TL ! muone vile !ovyoo
Nilishafanya hayo tayari katika utangulizi wa mada yangu
 
Mi nashauri mwaka huu vijana kwa wazee tukaTUBU jamaniii.....kutubu kuna maana kubwa sana kiroho na kimwili.
 
Back
Top Bottom