Uzi maalum wa maajabu mtaani kwako

Uzi maalum wa maajabu mtaani kwako

mtunzasiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
1,446
Reaction score
988
Hapa ndipo tunakutana na kusema maajabu yanayotokea kila siku mtaani kwako au unapoishi ili tushangae pamoja, iwe ni siasa, ustawi wa jamii, maendeleo ya watu, maliasili na utalii, kilimo, sanaa au chochote cha kustajabisha kwa wengine,
Nianze mwenyewe nimejionea naona kila siku na kustajabishwa hapa kwetu kigoma mjini yaani jimboni kwa zitto, kigoma mjini imezungukwa sehemu kubwa na ziwa Tanganyika hilo sio ajabu ila ajabu kubwa wakazi wakaao karibu kabisa na ziwa Tanganyika yaani mama mita 1000 yaani km 1 tuu wanashida kubwa ya maji safi na salama kiasi maji hupatikana maramoja tuu kwa wiki wakati wanayo maji ya ziwa Tanganyika kama kilomita 1 tuu toka kwenye makazi yao yaani maeneo kama Ujiji Lubaga mpaka kibilizi, hiyo yote tisa lakini kumi wakazi hawa hawa wanaposhindwa kuvumilia uhaba huo wa maji hukimbilia ziwani, ama kufua nguo zao au kuoga na kujichotea maji, hapo napo ni shidaa maana ukikutwa na polisi ujue utaenda jela ama ulipe faini kubwa kwa uharibifu wa ziwa. Wewe mtaani kwenu kuna nini cha kustajabisha??? Tililika sasa........!!
 
Wamama kushinda kwenye duka la mwenzao bila kujua yupo kazini wao wanapoteza muda.
 
Mtaani kwangu makoka,kibangu anayeishi huku a like hapa nimpe maajabu
 
Mtaani kwangu kuna jamaa anatoka Kolomije lakini anataka watu wanaotoka mikoani waombe kibali cha kuja mtaani kwangu sasa sijui yeye kaombea wapi kibali alivyokuja kutokea kolomije.
 
demu wangu anakaa kwa mkua mwembeni pale
Hahaha mkuu safi sana sasa skia me visa vyangu vingi na maajabu ya masela wangu yanaanzia pale makoka mwisho kama unashuka kuja kibanda cha simu..lile pori lote la jeshi tuko sisi watoto wa mtaa siku ukija we ulizia tu namtafuta mubashara ndege john..hutaamini.
 
Hahaha mkuu safi sana sasa skia me visa vyangu vingi na maajabu ya masela wangu yanaanzia pale makoka mwisho kama unashuka kuja kibanda cha simu..lile pori lote la jeshi tuko sisi watoto wa mtaa siku ukija we ulizia tu namtafuta mubashara ndege john..hutaamini.
mkuu hilo jina lako linasaundi kijanja janja sana, malizia visa kwanza

halafu yale magari ya kwa mkua-ubungo nayo ni visa mubashara kabisa
 
mkuu hilo jina lako linasaundi kijanja janja sana, malizia visa kwanza

halafu yale magari ya kwa mkua-ubungo nayo ni visa mubashara kabisa
Hahahah kuna mlima fulani..kilimahewa ukipanda tokea makoka shule..hahah yale macoaster usishangae gear mbili inakataa kuingia sa inabidi dereva acheze vizuri maana gari linarudi nyuma kabisa ..kuepuka hilo mkuu uwage unapada noah tu
 
Back
Top Bottom