mtunzasiri
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 1,446
- 988
Hapa ndipo tunakutana na kusema maajabu yanayotokea kila siku mtaani kwako au unapoishi ili tushangae pamoja, iwe ni siasa, ustawi wa jamii, maendeleo ya watu, maliasili na utalii, kilimo, sanaa au chochote cha kustajabisha kwa wengine,
Nianze mwenyewe nimejionea naona kila siku na kustajabishwa hapa kwetu kigoma mjini yaani jimboni kwa zitto, kigoma mjini imezungukwa sehemu kubwa na ziwa Tanganyika hilo sio ajabu ila ajabu kubwa wakazi wakaao karibu kabisa na ziwa Tanganyika yaani mama mita 1000 yaani km 1 tuu wanashida kubwa ya maji safi na salama kiasi maji hupatikana maramoja tuu kwa wiki wakati wanayo maji ya ziwa Tanganyika kama kilomita 1 tuu toka kwenye makazi yao yaani maeneo kama Ujiji Lubaga mpaka kibilizi, hiyo yote tisa lakini kumi wakazi hawa hawa wanaposhindwa kuvumilia uhaba huo wa maji hukimbilia ziwani, ama kufua nguo zao au kuoga na kujichotea maji, hapo napo ni shidaa maana ukikutwa na polisi ujue utaenda jela ama ulipe faini kubwa kwa uharibifu wa ziwa. Wewe mtaani kwenu kuna nini cha kustajabisha??? Tililika sasa........!!