Uzi maalum wa sisi diaspora tunaoonewa wivu kisa tupo Ulaya au USA

Uzi maalum wa sisi diaspora tunaoonewa wivu kisa tupo Ulaya au USA

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Kutokana na wabongo wengi kutuonea wivu sisi waishi ulaya nimeona nifungue huu uzi ili nyie mlioko nchi za maziwa makuu mje humu mumtaje mwana ulaya mmoja mkimtaka atoe uthibitisho wa yeye kuwa mbele USA au Europe.

Nimegundua wabongo wengi mna wivu mtu akiwa mbele mnamchukia mtamfukunyua mpaka akose raha duniani.

Haya Mimi Niko italy kiranga USA gentamicine rwanda Bibi faiza alikuwa Canada nk.

Kumbuka Kama hujawahi toka nje ya bongo sio laana.

Superbug.
 
Sawa, tumekusikia na tumewajua mnaoishi nje ya nchi mkuu, maswali yangu ni haya:

Mnafanya kitu / vitu gani kuwasaidia vijana wanaotamani / Wanaotaka kwenda huko nje?

Ukitizama nchi zingine kama Nigeria, Ghana, Senegal n.k akitoka mtu mmoja Hua ni mlango kwa wenzie nyuma, toka mmekwenda huko hata mwanafamilia achilia ndugu yako umewahi kumpa channel ya kufika huko? Au ndio ile kibongo bongo akipata atajiona?

Nini faida mpaka sasa ambayo umeipata / mmepata toka kwenda huko ambayo sio personal, kwa watu wengine? Wamefaidikaje na wewe / nyinyi kuishi huko?

Maswali mengine wataongezea wanajukwaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyani nyabu Yuko Ikungulyabashashi ana kilinge, ni Sangoma

Dah! Gile umeniwahi 😂😂.

Ile najiandaa tu kuandika ‘mimi nipo Ikungulyabashashi...paap....naona bandiko lako.

Ikungu all day everyday and twice on Sunday baby.

0F4ABDD6-3F8B-4508-8EA8-EB9D595DCCB1.jpeg
 
Hahaaaa em nicheke kidogo, uku nikijiuliza sasa kama mtu huishi Tanzania kuna haja gani ya kuja kusema huku na wakti unafahamu watu watakubishia na ina faida gani watu wakijua unakoishi, na kama wewe umeona kuna ulazma wa kusema si uweke vithibitisho wanavovitaka... Nimeona mmoja amesema hajaona haja ya kuweka ivo vithibitisho,, namuuliza sasa kulikua kuna haja gani ya kusema ulipo???

...😉take it easy...
 
Ulimbueni,watu wamekwenda viwanja kitambo ,na sasa wameumzika TZ wanaendelea na maisha ,wala hawajigambi,
kusafiri si fahari, fahari kufanikiwa na kuyapatia maisha.
Mabaharia wengine wanazungusha kete tuu huko ,kila siku wanakurupushana na Polisi
Eti hayo nayo maisha?
 
Mimi nipo nje ya nchi ya tanzania huku mbagala rangi tatu kimbangulile mtaa wa goroka ......huku maisha swafiii sio kama huko tanzania kwa wabongo kwanza mvua ikinyesha balaaa tupu mitaro inajaa maji hakuna pa kupita yaani kuchafuuu daadek
 
Muwe inspired tu jaman makasiriko ya nn??
Binafsi am so inspired na sna jajimentiiii
 
Back
Top Bottom