Uzi maalum wa Tanzu za fasihi

Uzi maalum wa Tanzu za fasihi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Fasihi Simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. TUKI (2004) Fasihi Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili.

Hivyo basi Fasihi Simulizi ni fasihi inayotokana na maneno ambayo huzungumzwa, hutolewa au kuimbwa ambapo mtungaji na mwasilishaji hutumia sanaa.

Tanzu ni istilahi inayotumiwa kuelezea au kurejelea aina ya kazi mbalimbali za kifasihi. Inawezekana utanzu mkuu kuwa na vitanzu vingine mbalimbali kwa mfano, tanzu kuu za kifasihi ni Riwaya, Tamthilia, Shahiri, Novela, Insha na Hadithi.

Vipera ni dhana inayotumiwa kuelezea vijitanzu katika fasihi hasa fasihi simulizi. Mfano: semi methali, mafumbo, vitendawili nakadhalika.Tanzu za fashion hujumuisha kazi za sanaa zifuatazo:-
HADITHI
SEMI
USHAIRI
SANAA ZA MAONYESHO
Ngano
Methali
Nyimbo
Majigambo
Tarihi/visakale
Vitendawile
Maghani
Tambiko
Visasili
Misimu
Ngonjera
Miviga
Soga
Mafumbo

Michezo ya watoto
Visoga
Lakabu

Ngoma

Misemo
Mizungu

Utani
Kupitia uzi huu karibu kushiriki kuweka kazi yoyote ya sanaa iliyokufurahisha sana ambayo unadhani tutaifurahia.
 
Back
Top Bottom