Wapenzi wa vyakula, habari zenu!
Hivi ukiambiwa vyakula vya Pwani, lazima kuna chakula kinachokujia kichwani haraka. Iwe ni pilau, biriani, wali wa nazi, samaki wa kupaka, urojo, viazi vya karai, vitumbua au mkate wa sinia, kila kimoja kina ladha yake!
Sasa hebu tujuane kupitia mapishi yetu. π
Nipe majibu ya haya maswali matatu;
- Ni chakula gani cha Pwani ambacho unaweza kula kila siku bila kuchoka?
- Kati ya pilau na biriani, unachagua kipi? Na kwa nini?
- Una siri gani ya kufanya chakula cha Pwani kiwe kitamu zaidi? ni tui la nazi, viungo au ni mbinu tu za kupika?
Na kama kuna chakula cha Pwani ambacho umekuwa ukitamani kujua jinsi ya kukipika, kitaje hapa ili wadau wenye ujuzi watufundishe.
Karibuni jikoni, wakuu! Leo tunashibishana kwa maneno, lakini tusisahau kushibishana kwa mapishi pia