Uzi Maalumu: Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda

b5-click

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
2,195
Reaction score
2,109


Karibu katika Uzi maalumu wa kilabu ya mpira wa miguu ya Ndada toka Mkoani Mtwara.

Jina la timu: Ndanda Fc

Jina la utani: Ndanda Kuchelee

Uwanja: Nangwanda Sijaona

Watazamaji:15000

Mkoa: Mtwara

Mdhamini: Kampuni ya Matairi ya Binslum
 
Timu imecheza dhidi ya Azam Leo pale chamanzi complex imepoteza mchezo lakini imecheza soka la kuvutia sana, imetengeneza nafasi chache na ikashindwa kuzitumia.
 
Hata Mimi pia, hasa pale mwisho.... Ilikua ni pigo huru la Penati ya wazi kabisa..
 
sijaridhika na mwamuzi wa mchezo huo

Tanzania hatuna waamuzi wa mpira wa miguu, yaan yule refarii ndio amenichefua sana jana.
Sijui ilitakiwa mchezaji wa ndanda atobolewe tumbo ndipo yule mwamuzi angejua kuwa ametendewa madhambi!!!
 
Wapenzi,mashabiki na wanakabumbu wote... Timu yenu ya Ndanda F.C Leo inacheza dhidi ya Ruvu stars pale Nangwanda sijaona... Kila la kheri NDANDA KUCHELE
 
Sare ya bila kufungana pale Nangwanda Sijaona... Timu imecheza soka maridadi sana... Tuna alama 23. Kibindoni

Hongereni NDANDA F.C
 
Hawa Wamakonde huwa hawashindi game za nyumban, sijui kwanini???
 
Hawa Wamakonde huwa hawashindi game za nyumban, sijui kwanini???

Kweli ni katatizo haka.. Lakini heri nusu Shari(sare) kuliko Shari kamili(kufungwa)... Vijana wetu wakomae VPL tamu
 
Msimu huu wa FDL tumefanya usajili wa kuongeza wakongwe. Henry Joseph na Mrisho Khalfan Ngassa wakiwemo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…