Uzi maalumu kwa historia na maana ya vituo vya magari, daladala, na baadhi ya majina ya watu kwanini yalitumika kama kielelezo cha sehemu husika.

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Salaam wakuu.

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Majohe "KWA NGOZOMA"
Huyu ngozoma nasikia yupo mpaka leo na ana bucha lake, alikuwa mfanyabiasha na alifungua duka kubwa sana maeneo hayo ya majohe wakati panaanzishwa miaka ya 2005 hivi.

2. Kwa Azizi Ali (Anayejua atuambie )
3. Kwa mpalange (jina maarufu sana hili) Huyu mpalange ni nani ?
3. Ile hospitali ya wazeeiya kwanini iliitwa mze.... (Kwanini isingeitwa nyerere, maana ukiwa tu umekaa zako makumb..... vijana wengi sana wanajifanya ni wazeeiya) Mods naomba nilinde hapa usifute uzi wangu)
4. Pale ukonga Banana kwanini panaitwa Banana )
5. Mbagara rangi tatu ( hizi rangi tatu ni nini zilikuwa zina maanisha nini )
6. Mbeya mafiati, kwanini paliitwa mafiati wakati tunajua FIAT ni aina ya gari.

Mengine naomba mjazie.

Ahsante
 
2. Kwa Azizi Ali. Azizi ali ni jina la AGP wa kwanza wa polisi. alikuwa akiishi maeneo hayo. Historia ipo humu humu. ngoja wazee waje wataeleza kwa undani zaidi.
 
Umesahau kwa inch tisa watupe kisa chake hiki kituo pale jf ilikuwaje pakaitwa hivyo.
 
GANGILONGA Iringa mjini Neno GANGILONGA kwa Lugha ya kihehe ni JIWE KUONGEA ndio sababu ya eneo Hilo kuitwa jina hilo

GANGILONGA JIWE lililoongea kwa maelezo ya wazee wetu wa kale
 
Hii nimeisikia sana hii, Ahsante sana Kaka
 
Kwa Mama Chibonge na kwa Mpalange
Hawa watu wana ukubwa gani huko...?
 
Mafyati ilikuwa ni sehemu ya stendi ya magari ya zamani marefu ambayo yalikua yana beba vitu mfano tax au nondo zile ndefu kwa hiyo yalikua pale ndo yanasimama ndo wakapaita stendi ya mafyati
 
Tandale kwa Bi Nyau
Kwa mworombo r-chuga
Kwa matojeo r-chuga
Kwa ndevu tegeta
Masika - morogoro
 
Makoroboi, mchafu kuoga,...
Mwanza
makoroboi . jina hilo linatokana na watengeneza vibatari maarufu (koroboi) walikuwa wanatengeneza koroboi hapo. mpaka sasa wapo japo siku hizi hawatengenezi kutokana na ujio wa taa za kichina hizi za kuchaji. ila wapo humo kwa ndani wanatengeneza matranka ya wanafunzi.. kuhusu mchafu kuoga(mto milongo au mto kenge) ni jina linalotokana watu waliochafuka walipenda kwenda kuoga humo mtoni na kujisafisha zamani kidogo ambapo maji safi ya bomba yalikuwa changamoto. vituo vingine maarufu 1. Natta - jina la hotel iliitwa natta hotel kwa sasa ni maduka mbalimbali na kuna chuo na kanisa hapo. mlango mmoja- soko la wamachinga , hili soko lilikuwa club ya pombe za kienyeji kulikuwa na mlango mmoja tu wa kuingia humo. baadae serikali ilibadilisha na kuwa soko la wamachinga. sinai- hili jina linatokana na garage ipo hapo pembeni .
 
Shukran nyingi kwako
 
Shukrani sana mkuu
 
Back
Top Bottom