Uzi maalumu kwa tulio kulia kijijini

Uzi maalumu kwa tulio kulia kijijini

Mowwo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
1,083
Reaction score
1,628
Nawasalim wanaJF.

Kwema? Je umekulia mjini au kijijini?
Nimekumbuka enzi hizo maisha ya kijijini yalivokua nikaona nishee na wadau. Kwa tulioishi au kukulia kijijini kila mmoja anakumbukumbu ambayo akikaa anaweza kukumbuka kua mazingira ya kijijini ndo yaliwezesha hiyo kumbukumbu. Nikimaanisha huenda angekua mjini asingekutana na hiyo memory kabisa. Yapo mambo kadha wa kadha lakini ngoja nishee yangu kidogo.

1. Thamani ya kula ubwabwa/ wali/ cheka na watoto

Sikukulia katika mazingira ya kula wali(chakula pendwa) mara kwa mara. Home ilikua ni ugali zaidi, kwahiyo siku ubwabwa unapikwa mara 1 kwa mwezi hiyo siku sichezi mbali, nikitumwa naenda chap kwa haraka, nakua msafi~yaani naoga mapema. Nakua na furaha sana. Baada ya kusafiri nilivomaliza darasa la 7 miaka ya 2000s mwanzoni kwenda Daslam nikakuta wanaupika kila siku jioni na wanaona kawaida. Basi sikutaman kurud na wakat wa kurud kijijini ulipofika niliumia sana. Siku hizi SIONI kama wali unathamani ilee.

2. kuparty haikuwa club wala ukumbini
Tofauti na maisha ya mjini sherehe zilizokuepo ni za Harusi au ubarikio na sikukuu za mwisho wa mwaka. Hizi zote zilikua zikifanyika nyumbani kwa wahusika. Malijendi tulikua tunatoka home na mfuko wa malborro/rambo kwaajili ya kuzamia ili kuweka msosi na kwenda kulia nje ya eneo la tukio. Siku rafiki angu alikamatwa na akanitaja kua tulienda wote kula msosi harusini nilikula mboko za kutosha.

3. Kulikuwa hamna TV wala umeme
Palikua na sehem moja tu mbali kidogo na home ndo tulikua tukienda kuchek video wakati wa sikukuu tu. Hiyo siku ndo siku pekee mwaka mzima ya kuchek kina komandoo kipensi, shozniga,rambo,vandame...nk Ruhusa ikitoka basi tunafurahi sanaaa

4. Kuogelea ni mtoni, mipira ya miguu/ football ni ya kusuka kwa makaratasi
Hamna swimming pool. Kuogelea ilikua marufuku mtoni lakini lazima kutafuta namna kutoroka home ili kujaribu kujua kuogelea mtoni. Tuliwahi kukamatwa mara moja mimi na rafiki angu tukafinywaa. Mpira wa kuchezea unasukwa fresh unatumika mpk ukichoka unasukwa mwingine na tunaenjoy balaa mpk watoto wa walimu.

Yapo mengi sana yakushea km kuwinda, kazi za shamba,utukutu shuleni,ugumu(kukataa kuoga😀) lakini pamoja na kua palikua kijijini hamna mazingira kama ya mjini ila Maisha yalikua ya furaha sana. Vyote naona vilikua wonderful memories.

Wale waliokua wakiishi mjini share experience yako wakati ulipofika kijijini. Share nasisi wadau kitu gani ulifurahia kipindi unaishi kijijini kwako hapa👇
Villa (1).jpeg
 
Kwenda porini kutega ndege. Kutoroka hom usiku ili kwenda disco.Kumfuatilia demu wa Kijiji Cha mbali siku ya gulio. Kupanda juu ya mwembe/mchungwa na kula matunda yake huko huko juu.
 
Kwenda porini kutega ndege. Kutoroka hom usiku ili kwenda disco.Kumfuatilia demu wa Kijiji Cha mbali siku ya gulio. Kupanda juu ya mwembe/mchungwa na kula matunda yake huko huko juu.
😀😀unaeza usile chakula mchana ukala matunda tuu. Dem wa kipind icho wa kijijini unamfkuzia tu ila kukutana nae wawil ishu
 
Back
Top Bottom