scooby huwa ananogesha sana movie, muvi nyingi ni mtu huwa yupo loyal lakini tamaa ya pesa inamsumbua, hata akizioata haridhiki na ndio lunaenda kuwa anguko lake.
mara ya mwisho nimecheki dili za mchongo, skubi yupo na genge lake linaitwa mazombi 😂😂
dark master huwa ni mtoto wa mjini mwenye mishe za kufukuzia fursa kwa namna yoyote, sahau kuhusu loyalty hapa kama ni partner wake,
kuna dem nae naanza kumuona siku hizi yupo kwenye changudoa mchanaji, kama bongo hood ni chai na mkate basi yeye ni blueband, anauvaa uhalisia fresh.
mapacha wawili ni wazee wa kazi chafu wanafuata order za boss wao kuua maadui zao, yani ni ngumu sana kuwachomoka.
one the incredible aliacha lakini ndio aliefungua milango kwenye bongo hoods, huyu naweza kumfananisha kama sugu alivyo lwa bongo fleva.