UZI MAALUMU: Vyanzo zaidi vya mapato na tozo kwa Serikali vipo vingi sana

UZI MAALUMU: Vyanzo zaidi vya mapato na tozo kwa Serikali vipo vingi sana

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Tuache utani hii serikali inachapa kazi jamani, raia wako very happy wanasema mama anaupiga mwingi hadi unamwagika, Mungu awape nini watanzania kupata Rais ambaye anachapa kazi masaa 24 kwa ajili yao halali kabisa.

Tuache kulalamika kuhusu TOZO , vitu vidogo sana ni lazima serikali itoze tozo ili kuleta maendeleo asiyetaka ahamie Burundi

Uzi huu ni maalumu kwa serikali yetu pendwa tuikumbushe pale inaposahau vyanzo vya mapato na tozo. mimi naanza na hivi siku ya leo

Tozo ya bando ni ndogo mno jamani, atleast mb 1000 ingekuwa ni tshs 3000 maana ukiangalia kwa afrika bado sisi tunachaji nafuu sana , hapo serikali inapoteza mapato sana.

Sabuni za kuogea, mafuta ya kula, chumvi,viberiti...hapo serikali iongeze tozo ya sh 50 kwa kila bidhaa itakayouzwa, ni chanzo stable sana cha mapato hapo.

Kila mmiliki wa laptop na computer za desktop alipie tshs 1000 kwa mwaka kwa kila mashine.

Tozo ya baiskeli irudi, tshs 1000 kila basikeli kwa mwaka.

Ongezea zako please, hii ni nchi yetu tuipende sana kwa kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa na waziri wake wa fedha katika kubuni TOZO mbalimbali kwa ajili ya mapato
 
Meza
Viti
Makochi
Mapazia
Dinning table
Vitanda
Mashuka
Mapazia
Vyandarua
Wardrobe
Milango
Madirisha

Hivyo vyote ni vyanzo vya mapato, haiwezekani kama wewe ni mzalendo umiliki hivyo vyote kisha usivilipie tozo.
 
Nimecheka sana, halafu kodi ikikusanywa wakati wa kutoka unaambiwa ni pesa ya rais!
 
Kodi ambayo inapotea Bure ni hii ya kukomenti jf,twita,insta bila Kodi..waweke japo TSH 50 Kwa thread au komenti Moja kwenye mitandao ya jamii
 
Back
Top Bottom