Uzi maalumu wa kujimwambafai

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
habari madingii na mazeri,bila kuwasahau machalii,


Moja kwa mbili niwaite hapa katika duara hili tujumuike kulizunguka huku tukiwasha moto katikati ili kupunguza baridi kali inayoambatana na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita za kumaliza kisahani kwa sekunde.

Unajua mwamba maisha ni kama sigara au fegi unapopiga pafu moja nayo inasogelea kaburi lake huku ikitamani iendelee kubaki ikining'inia katikati
ya vibanio vya mdomo wako nawe ukitamani kuipoteza kabisa katika ramani ya sayari ya dunia,kwa utamu wa moshi wake huku ukisahau kama unachoma mapafu ya mkeo, watoto au familia unayokutuma mkate wa asubuhi na jioni.

Ok, sasa mwamba si unajua kujimwambafai sio poa usawa huu watu tumepinda kama mizengo, ukizingua tutakuachia mapengo haijalishi uko dabo
ama singo...hizi sio siriz zisizokwisha kama isidingo....Siku moja niliji ''mwambafai mwambafai'' kwa mapoti flani walinikamata kwa kosa la kubaka panzi
wakaniachia bila kutoa faini yeyote na wakanipigia saluti wakidhani nipo kitengo kumbe ni mpambe wa bosi.

Sasa nisimalize maneno nikakosa ya kuongea tumoro, nawe tumia ''mwambafai mwambafai'' kutupa ujumbe wenye kuelimisha jamii iliyopotea.
 
Siku moja niliji ''mwambafai mwambafai'' kwa mapoti flani walinikamata kwa kosa la kubaka panzi.

Jamaa inaelekea unapiga sana pombe.
Ungezama kwenye Uzi wa Baba lao Mshana Jr
 
Siku moja niliji ''mwambafai mwambafai'' kwa mapoti flani walinikamata kwa kosa la kubaka panzi.

Jamaa inaelekea unapiga sana pombe.
Ungezama kwenye Uzi wa Baba lao Mshana Jr
Ntakuverifai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…