Fursa ni kulingana na sehemu ulipo, kama ni biashara hizi za kawaida uza chakula, nafaka au vyakupikwa huwezi kukosa riziki.
Nyingine ni kilimo hapa inabidi ujifue kweli kweli, kujifunza, mtaji na usimamizi. Binafsi ilinichukua miaka mi3 kuanza kilimo tangu niliponunua mashamba. Faida ipo ila sio kama zile calculations za motivatinal speakers, na inahitajika kujifunga mkanda kweli kweli, kwangu kilimo imekuwa sehemu yangu yakuongeza kipato na kutengeneza mitaji yakuongezea kwenye hizi formal business nizifanyazo mjini, naweza nisichukue mkopo wowote kukuza vijibiashara vyangu shamba likanisaidia kufanya hivyo.
Kingine kufanya biashara zinazowahusu wanawake, si unawajua muda mwingine ni bora wasile ila wavae vizuri, kunukia, kusuka n.k