UZI MAHSUSI: Zilipendwa, audio/ video/ mashairi lyrics). Karibu upate burudani.

UZI MAHSUSI: Zilipendwa, audio/ video/ mashairi lyrics). Karibu upate burudani.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Huu ni Uzi maalum wa kupata flashbacks za nguvu kutoka nyumbani Tanzania Na hata nje ya Tanzania.

Karibuni kwa audio, video Na lyrics..
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=Qc7M0ljsAXI&pp=ygUYZmF1bGF0YSBqdXdhdGEgamF6eiBiYW5k


[FAULATA - Juwata Jazz Band]
(Kibao kimeimbwa naye mwenyewe Joseph Lusungu , Moshi William, Suleiman Mbwembwe, Joseph Maina,
Juma Akida Hamisi Kitambi na Tino Masenge, solo chini yake Mabera, rythim na Pishuu, bass na Issa Ramadhani,
drums kucharazwa na Saidi Mohamed, Mohamed Haroub kwenye tumba, Julius Betto na Zitto Mbunda kwenye trumpets,
Mnenge, Abdi Mketema na Hagai Kauzeni kwenye midomo ya bata (sax) )

(Mwanzo)
Ilikuwa siku ya jumanne asubuhi
nataka kwenda kazini
ndipo ulipotamka neno kuwa umechokaa
kuishi na mimi

kosa gani eh
ewe Faulata
sikupata jibu jengine ila sikutaki eh
sikutaki tuuu

kuchunguza kuchunguza kumbeeeeee
umempata awezae kumiliki maisha yako
kunishinda mimi

[wote] Kibwagizo
ama kweli oh maradhi yote ugua
lakini kuchacha usiombee

[Lusungu]
naomba unisikile kwa makini
haya ninayokuambia
kuibuka na kuchacha mola ndiye mpangaji wa yotee

[wote] kibwagizo

[Lusungu]
umekuwa kama mzigo wa moto ..... lo salale
haubebeki wala haushiki
nakuruhusu wendee ....... nenda
utaiona dunia eh

[wote] kibwagizo
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=XFsmh1S19us
[ASHA MWANA SEFU - Juwata Jazz Band]



Asha mwana Sefu

niambie mpenzi wangu

imekuwaje leo mama upo kimya hivyoo

ni lipi jambo lilokuudhi nieleze leo

sema Asha sema sema mpenzi wangu

kama mimi nimekuudhi unielezee



nashukuru mume wangu

kwa kuniulizaa oh

unakunywa pombe uonekani hata siku tatu

nachekwa na wenzangu

watoto wanateseka

hata huruma huna

kwa hawa malaika



(wote) kibwagizo

ulevi ulionao bwana unanitia aibu

huna mapenzi eh

kwangu mimi na watoto



(TX)

ah mama nimekubali

maneno yako mama ....... oh mama

wakale walisema

mjinga pa kwenda

pa kurudi anajua

pabaya na pazuri nasema



(wote) kibwagizo



(Zengakala)

natubu mbele yako

na hata kwa hao malaika

unisamehe duniani

hata mbinguni ...... oh oh



(wote) kibwagizo
 
Buji🔥🔥 hivi mistari hii ...hata majembe hutokea wakati Fulani kugongana,sembuse Mimi na wewe! Yapo ktk wimbo gani wa Msondo!
 
[MSAFIRI KAKIRI - Juwata Jazz Band]

(Utunzi ni wake TX Moshi William, solo kupigwa na Abdi Ridhwan 'totoo' au siku hizi Pangamawe,

rythim na Pishuu, bass na Issa Ramadhani. Katika wimbo huu Sax zimepulizwa barabara kabisa na Mnenge,

Abdi Mketema, na Hagai Kauzeni)


(TX Moshi)
Mini mwendapole ninakuja
msafiri kakiri
walisema waswahili nenda ukitizama mbele na nyuma

moyo wanidunda nilidhani
tena kwa uoga wa safari
yakutafutaa
maisha mazuri
najikaza kiume nakwenda
nawapisha wenye haraka
waje wapite mimi naja taratibu

oh Ridhwani sema

najikaza kiume nakwenda
nawapisha wenye haraka
waje wapite mimi naja taratibu

(sax murua)

(wote) kibwagizo
msafiri kakiri .....kakiri
mwendapole ninakuja
nawapisha wale warudio na waendao kwa haraka

(Lusungu)
safari ni hatuaa
mwenda pole hajikwai
penye nia pana njia
lengo langu litafikia eh

(wote) kibwagizo

(Lusungu)
kwa kuwa duniani
kuhandaika ili ufanikiwe
pasi nitasafiri kila pembe
iko siku mungu atanisaidia eh

(wote) kibwagizo

(Lusungu)
Mwendapole hajikwai
akijikwaa haanguki
akianguka haumiii
kuumia kwake kidogo tu

(wote) kibwagizo

(Lusungu)
kwa kuwa duniani kuhangaika ili ufanikwe
basi nitasafiri kila pembe
iko siku mungu atanisaidia eh
 
Back
Top Bottom