SoC02 Uzi unafuata sindano

SoC02 Uzi unafuata sindano

Stories of Change - 2022 Competition

ponerad

Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
6
Reaction score
6
Katika maisha yetu ya kila siku tumekua tukisikia au tukikutana na maneno kama haya kuwa Ukitaka kufanikiwa lazima uwe na vitu kimoja wapo kati ya hivi vichache kama

1: BAHATI
2: KIPAJI
3: ELIMU

Ingawaje kitu kinachoitwa KONEKSHENI ni muhimu zaidi ya hivyo vyote.

Tumekua tukisikia hadithi mbalimbali mitaani ambazo zimekua zikikatisha sana tamaa hasa kwa vijana wetu waliobahatika kusoma na kumaliza elimu za juu bila kufanikiwa kupata nafasi za kazi. Tumekua Tukisikia maneno kama, "...unasoma ili uwe nani??..walikuwepo wenzako. Wasomi wenzio wanazunguka na bahasha kutafuta kazi na hawapati. Mara kuna mwenzio ana masters analima nyanya...''

Kwa kweli unaposikia habari kama hizi ukiwa kama kijana lazma uvunjike moyo na kujikuta unachukia mfumo wa Elimu na kuichukia serikali yako kuwa haifanyi chochote kwa ajili ya vijana.

Mwaka 2015 nimemaliza Chuo nimerudi Nyumbani nikiwa na shahada yangu ya BIMA na udhibiti wa majanga nikakutana na rafiki yangu mmoja anaitwa Edwin Luoga ambaye huwa tunataniana nae sana, yeye ndio alikua anaanza mwaka wa pili anachukua shahada yake ya Mipango miji.

Akaniambia Ponera wewe unasoma soma tu vitu visivyo na maana, mzee wako anafanya kazi Tanesco halafu wewe unasoma masuala Ya BIMA ili iweje? Una Nani anafanya kazi pale Bima atakayekushika mkono au umesahau UZI UNAFUATA SINDANO.

Kama mzee wako yupo tanesco wewe ilibidi uende hata VETA usome hata cheti cha ufundi umeme ili upate KONEKSHENI upate mchongo Tanesco kupitia mzee wako.

Kiukweli sikumjibu kitu nikanyamaza tu ingawa hayo maneno yaliniumiza kiasi chake nikaamua kubadili aina ya maongezi.

Nikakaa mtaani mwaka mmoja bila kazi ilipofika 2016 nikaamua kumuomba mzee wangu Anilipie Ada nisome Stashahada ya uzamili katika Elimu yaani PGDE kwani watu wengi walikua wakisema kuwa Ukisoma UALIMU basi ajira ni nje nje unapangiwa tu kituo unakula maisha🤓.

2017 nikamaliza nikakaa mtaani sikupata kazi kila nikiomba nakosa mpaka 2019 mwishoni nikaja kupata kazi shule binafsi napo nikafanya mwaka mmoja tu tukatimuliwa kutokana na maneno maneno na roho mbaya za waajiri wetu🤣.

Ki hela nilichokua nakiwekeza kidogo kidogo nikaamua kutafuta Line za uwakala nianze biashara ya Kuweka na kutoa Hela (mpesa,tigopesa,airtel money,ttcl pesa na halopesa na kuuza vocha).Nilianza na Milioni moja kamili lakini kutokana na ujana mambo mengi nikajikuta kila siku mtaji unashuka tu mara imebaki laki 8,mara 6,mara laki 3 nikaamua kulewea pombe hela yote nikabaki 0.

Hapo nyumbani kwetu wanajua mimi nafanya kazi ya ualimu kumbe nilifukuzwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja nyuma ila sijasema chochote kwa sababu naishi tu mwenyewe ghetto.

Aliyekua ananiokoa na kunilealea ni mama mtoto wangu ambaye yeye alikua anafanya kazi hoteli moja kubwa hapa mjini kwa hiyo tukawa tunakula na kulipa kodi kwa kupitia mshahara wake.

Mwaka 2021 mwishoni nikaamka tu asubuhi nikiwa kama sijielewi elewi nikaamua kwenda stationery nikalipia nikaanza ku type cv palepale nikatoa copy za kutosha nikaandika na barua ya kuomba tu internship maana siwezi kuomba kazi moja kwa moja kwa kua sina uzoefu wowote kwenye suala la BIMA nikaandika barua zaidi ya tano nikatoa copy ya CV na vyeti za kutosha nikanunua na bahasha nikaziweka kisha nikaandika anuani za mashirika mbalimbali kama Shirika la bima la Taifa (NIC), NHIF, NSSF, CRDB, NBC na PSPF nikiomba Internship kwenye kitengo cha bima halafu nikazielekeza kwa mameneja wa matawi husika kisha nikaenda Posta nikanunua Stempu ili nizitume kupitia posta kwani niliogopa kuzipeleka kwa mkono kwa kuona aibu kuongea ongea na ma sekretari kwani wanakuwaga na maswali maswali ya kujua undani wa mtu na kutaka mtu uchoreke tu bure.

Nilikaa miezi kama mitatu bila kusikia chochote kutoka popote pale nikazidi kukata tamaa kabisa na kuona kama nimepoteza muda kabisa kwenye suala la kusoma bora ada yangu ningepewa tu mkononi nikafanya biashara basi.

Kuna siku moja nimelala zangu barazani asubuhi nikapokea SMS ya kawaida ikisema,"ponera leta matokeo yako hapa Crdb tawini.Nikastuka nikampigia hakupokea baadae akanipigia akasema umetuma maombi ila hujaweka cheti cha matokeo (academic transcript) fanya ulete hata tawini.

Nikafanya haraka nikaenda kukitoa copy nikapeleka akasema sawa vimefika tutakutaarifu.Nikasali sana siku ile nikisubiri simu ya yule mtu huku namba yake nikiwa nimei save kabisa ili ikipita muda bila kunitafuta nimtafute.

Kesho yake tu akanipigia simu mchana,kabla sijaipokea roho ilikua ikinidunda vibaya mno.Nilipoipokea tu nikakutana na neno POLE SANA bwana Ponera😁😁

CV yako nimeituma makao makuu wameijibu wamesema wao wanachukua watu waliomaliza kuanzia 2019 na kuendelea mbele pia GPA yako ni ndogo sana sisi tunataka mtu Mwenye GPA ya 3.5 kwenda juu,kwahiyo pole sana na usikate tamaa tafuta sehemu nyingine, kisha akakata simu😭😭.

Kiukweli moyo ukawa wabaridii nikajikuta natukana kimoyo moyo nikijisemea sasa alikua na sababu gani ya kunipigia si bora angekaa kimya tu maana siku zote ukiona kimya tayari unakua ushapata majibu mwenyewe.

Nikasema mimi ndio basi tena siwezi kupata tena kazi kama mifumo yako ndio hii ya kuangalia GPA.

Nikaamua tu kuendelea na maisha yangu ya kuunga unga na Washkaji zangu tukipata chochote tunakunywa pombe basi kuondoa tu mawazo huku tukupiga story za kuendelea kuilaumu serikali kwa mifumo yao mibovu na kulaumu tu viongozi akija huyu tunaona bora yule aliyetoka.

Baada ya miezi 5 mbele nakuja kupigiwa simu mara ya kwanza sikupokea nikijua labda ni kati ya watu wanaonidai ila nilivyoona kapiga mara ya pili nikaamua kupokea akajitambulisha kama Meneja rasilimali watu kanda kutoka bank ya crdb akaniuliza mambo kadhaa likiwemo ombi langu la kuomba internship bank hapo nikamjibu ndio akasema sasa naandaa usaili ila utafanya kwa njia ya simu kisha akakata simu.

Baada ya siku mbili akanitumia sms akasema usaili utafanya kesho saa 3 asubuhi kaa sehemu yenye utulivu.Kiukweli nikawa bado siamini najua ni wale matapeli wa mtandaoni ambao baadae watakuambia utume hela ili wakupe kazi.

Nilichokifanya ni kuingia mtandaoni usiku kucha sikulala na Kuanza kusoma mambo kadhaa kuhusu bank ya crdb na kuielewa zaidi na kesho yake nikapigiwa simu saa 3 asubuhi na kufanyiwa usahili na Nikaulizwa mambo yaleyale niliyokua nayapitia mtandaoni usiku mzima.

Baada ya siku mbili yule mtu akanipigia simu asubuhi na kuniambia Hongera umefanya vizuri sana usaili wako hivyo nenda pale tawini kuna fomu za kujaza na kuzikamilisha leo hii kabla ya saa 8 mchana. Nikafanya hivyo kisha nikapewa mkataba wa miezi michache kwa ajili ya kufanya hii project nika saini kisha nikapewa mtu wa kunifanyia Training ya wiki kabla ya kwenda kuripoti kituo nilichopangiwa ambacho ni wilaya ya pembeni kidogo kutoka hapa mjini.

Kiukweli ni mwanzo mzuri wa Kuikuza taaluma yangu na kujuana zaidi na watu na kutengeneza KONEKSHENI ndani kwa ndani ambapo baadae inaweza kuzaa kitu kikubwa zaidi na zaidi.

Hivyo vijana wenzangu Tusikate tamaa kabisa kila kitu kinawezekana ukiwa na Imani tu Na sio kuamini yale masuala ya UZI UNAFUATA SINDANO. Unaweza ukaomba kazi ya utendaji kata ukakosa ila Ukaomba Kazi Bank Kuu ukapata.

🙏🏽💪🏾😁😁
 
Upvote 0
Back
Top Bottom