Uzi wa garage/ mafundi gari wazuri popote ulipo

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
6,682
Reaction score
11,461
Habari ya muda huu wana JF,

Naomba tupeane ujuzi wa maeneo wanapopatikana mafundi wazuri kwa vigezo vifuatavyo.

1. Ujuzi mzuri.
2. Bei nafuu.
3. Uaminifu.
4. Maeneo wanapopatikana

Itakua sio vibaya kama utaweka location na contact zao hapa.

Binafsi huwa natumia fundi mmoja yupo mikocheni karibu na kairuki ni muaminifu, bei nzuri ila kwenye ujuzi ndio janja janja nyingi mno labda umpelekee kwa service ya kawaida tu ila mambo mengine nilijuta.
 
Nenda Jerry Garage & Spare Parts Mikocheni Viktoria kama unaenda Kairuki njia ya kwanza kulia unaacha ya Kairuki unaifuata 0715666656
 
Hivi anayewauzia magari wasanii anaitwa nani? Maana wanatumia muda mwingi gereji kuliko barabarani......#Nunua gari mpya mkuu achana na screpaz.....Ukishaanza kulikorochoa gari kwa hawa mafundi uchwara wa mitaani ipo siku gari lako litaungua.
 
Hivi anayewauzia magari wasanii anaitwa nani? Maana wanatumia muda mwingi gereji kuliko barabarani......#Nunua gari mpya mkuu achana na screpaz.....Ukishaanza kulikorochoa gari kwa hawa mafundi uchwara wa mitaani ipo siku gari lako litaungua.

Mkuu gari mpya unamaanisha zero km? Watanzania wengi hatuna uwezo wa zero km. Pia fahamu hata gari likiwa jipya kuna matatzo ya kugonga, kujisahau service ukaua kitu, gari kuharibika kwa sababu mbali mbali n.k.

Unaweza kununua used car hapa bongo na usiguse garage zaidi ya service na ukanunua mpya zero km siku ya pili upo garage...
Just understand hizi ni machine....
 
Mkuu gari mpya unamaanisha zero km?
Hapana mkuu simaanishi 0 km namaanisha hizi tunazoagiza kutoka japani 2nd hand ambapo huku kwetu tunaita mpya,screpaz namaanisha hizi mikweche ya hapa TZ.
matatzo ya kugonga, kujisahau service ukaua kitu, gari kuharibika kwa sababu mbali mbali
Matatizo hayo mafundi wengi wapo haihitaji kuumiza kichwa.....Nilivyoona umeanzisha uzi wa kutafuta wataalamu wa ufundi nikajua hapa unatafuta mafundi wa kusuka engine,kusuka gear box,carburetor,timing belt etc ila wa services au kubadilisha kifaa kilichoaharibika hao wapo wengi sana!
 
Huu uzi ulikuwa ni muhimu sana, sijui kwa nini watu waliupotezea!
 

Kuna gari mpya isiyo na warrant Mzee baba?
Lazima utapewa miezi sita au 5,000km za uangalizi na free services.
 
Kuna gari mpya isiyo na warrant Mzee baba?
Lazima utapewa miezi sita au 5,000km za uangalizi na free services.
Magari mapya kabsa bongo kama sio la shirika flani au NGO basi ni la serikali au fogo mmoja hv town.

Uzi huu ni kwa sisi wa "new from Japan"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…