Bhagavan
JF-Expert Member
- Oct 28, 2017
- 1,946
- 2,822
Nianze kwa kuwapa pole wana JF wenzangu kwa majukumu ya kila siku, napenda kusema tuendelee kupambana na hali zetu pasipo kukata tamaa.
Lengo la kuanzisha uzi huu ni kutuoa yale ya moyoni. Tupo katika jamii ambayo ina watu wenye tabia tofauti tofauti, tuna ndugu jamaa na marafiki ambao wamekuwa na tabia ambazo hazitupendezi kwa namna moja ama nyingine hatufurahishwi nazo hivyo kupitia uzi huu kuliko kukaa nalo rohoni ama kumteta mtu funguka hapa tabia usizozipenda. Hii itatusaidia kujirekebisha kwani miongoni mwa tabia zitakazo semwa hapa inawezekana mimi au wewe tunazo hivyo tutajua ni jinsi gani tunavyowachukiza wanaotuzunguka.
1.Mimi kuna hii tabia huwa inanichukiza sana tena siipendi, Tabia ya kuombwa pesa na mwanamke kihasarahasara kisa tu ni mpenzi wangu, utasikia "baby NATAKA pesa ya mchango wa harusi".. Pambaaaf pesa yangu badala ya kuomba unasema "NATAKA"... Sipendi
2.Tabia ya washkaji kupigana mizinga kiholela holela, tupigane mizinga kwa sababu maalum unaumwa, umefiwa nk lakini sio "oyaa nitoe 5000 nipige hata BEER mbili mwanangu"... sipendi
Yangu mimi ni hayo. Sema na wewe usichopenda/kinachokuudhi
Karibu.