Uzi wa kubuni vyanzo vipya vya mapato visivyoumiza Watanzania

Uzi wa kubuni vyanzo vipya vya mapato visivyoumiza Watanzania

Akilindogosana

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2020
Posts
4,303
Reaction score
12,679
Huu ni uzi maalum wa kila mwenye wazo au chanzo kipya cha mapato kwa ajili ya serikali yetu ambacho hakitasumbua wala kuumiza watu. Maana hii kazi inabidi iwe ya Watanzania wote na inabidi uwe mjadala wa wazi mahali popote ili watu watoe mawazo ya kujenga nchi. Na sio kuleta kodi za kuumiza watu.

Karibuni watu wote mtoe na kubuni vyanzo vipya. Usiwe na hofu, maana wazo lako ni la thamani mno! Hata kama lina mapungufu watu wataliboresha. Usiwe na hofu wazo lako ni la muhimu na thamani kwako wewe na kwa taifa.

NB: KODI YA KWENYE MAKATO YA MIAMALA YA SIMU IFUTWE, NI MBAYA MNO NA HAINA STAHA KABISA.
 
Nimalo wazo la uhakika na uzoefu ninao lakini kwanza nipate mahala salama pa kuliweka, ili lisitafusiliwe vibaya, hakika litaleta Tija mabadiliko makubwa pande zote za kodi.
 
Ila tuambie kwanza kama ni mmoja wa mliotufikisha hapa, ili tusaidiane mawazo kwa nia njema.
 
Ila tuambie kwanza kama ni mmoja wa mliotufikisha hapa, ili tusaidiane mawazo kwa nia njema.
Mimi sipo huko. Nimeona bora nianzishe uzi bure ili tutafute suluhisho ambalo halitatuumiza. Haya mambo tumewaachia wanasiasa wasio na ujuzi na wala hawana uchungu na watu kwakuwa wanapata mishahara mikubwa 12m kwa mwezi na madili ya mabilioni.

Inatakiwa hili jambo la kutafuta vyanzo vipya vya mapato liwe jambo la watanzania wote kabisa. Hawa wanasiasa sio watu wazuri.

Ulalamishi hausaidii kitu, ni heri tuje na suluhisho. Tuelezee kwa kina juu ya vyanzo hivyo. Maana wanasiasa wetu wanatuletea matatizo.
 
Nimalo wazo la uhakika na uzoefu ninao lakini kwanza nipate mahala salama pa kuliweka, ili lisitafusiliwe vibaya, hakika litaleta Tija mabadiliko makubwa pande zote za kodi
Weka tu wazo lako hapa. Tuokoe taifa letu yaani wazo lako ni la thamani kubwa mno.
 
Ni kwa vile Serekali haina ubia na Dini vinginevyo ningeshauri kuwe na kodi kwenye fedha za Sadaka makanisani au kodi ya mapato ya michango kwenye nyumba za ibada.

Kwenye miamala ya simu iliyo chini ya elfu 50 isiwe na kodi.
 
Hakuna kodi iliyowahi kukubaliwa hata siku moja.
kodi ni must itozwe ama tutake au tusitake.

ulalamishi hauwezi kukoma.
Nakuona "Mwigulu" umekuja kujitetea hapa na ID nyingine.

Halafu wewe lazima uwe MTU MZITO SANA SERIKALINI NA UNAPOKEA MSHAHARA MKUBWA MNO KWAHIYO KODI HAIKUUMIZI KABISA.

Poa mkuu endelea kutuchora.
 
Waweke road tolls waruhusu daladala kwenye mwendokasi zipige express routes during rush hours maybe saa 11-3 asubuhi kwa level seat ya buku buku! Na saa 10-3 usiku!

Dereva aache buku kila trip kwenye starting point! Hizo buku buku ziwe kama kodi ya wazalendo!
 
Rasilimali zetu za asili zimeisha? hebu tuanzie hapo kwanza!
Ndugu yangu haya mambo hayana wepesi huo.

Rasilimali ni jambo moja mavuno ya rasilimali ni jambo jingine.

Extraction ya gas, nikel & yanataka mitaji mizito.

Anyway tutafika tu.kama ni touarist attraction hakuna nchi isiyonayo

Hata watalii nao ni wa kuwagombania. Katikakati ya covid hii chumi nyingi zimeanguka.

Ili kupata recovery ya dharura lazima lazima mbanane humohumo kwny locally based collections
unless irudi kufanya biashara mojamoja
 
Back
Top Bottom