1. Rais na Majaji waanze kulipa kodi
2. Serikali iache mchezo, iwabane kweli wafanyabiashara walipe kodi, Wafanyabiashara wengi wanachezea EFD machines, hawalipi kodi.
3. Kariakoo kuna Wachina wanaendesha biashara , wanasuply mzigo kwa wafanyabiashara wa Kitanzania na wa nje na Wachina hawa wanakwepa kodi ajabu. Ukimuambia naomba risiti ya mzigo wangu anakwambia ondoka hata mzigo wenyewe uache!
4. Serikali iboreshe mifumo, yaani watu wahimizwe kutumia cashless system. Kwa sasa hivi tuna cashless system kama vile M-Pesa, Tigo Pesa etc, lakini hizi ziyo rafiki sana wa kufanya biashara sababu ya Makato na siyo userfriendly kivile. Serikali Itengeneze mfumo kama wa Wachina wa WECHAT MONEY ili watanzania waanze kuuziana bidhaa kupitia cashless platform. Kwa mfumo huu mapata yaserikali yataongezeka hata mara TATU kwa sababu hata buashara ndogondogo zitavutiwa kutumia huu mfumo na matokeo ya serikali itaongeza uwanda wa kodi kwa kiwango kikubwa sana. Mwigulu sikia, Fanya juu chini uintroduce kitu kama WECHAT MONEY nchini. Lakini hakikisha inakuwa owned na kampuni ambayo serikali itakuwa na shares nyingi sana.
5. Tuna vyanzo vingi vya utalii, tuna milima ambayo haijaendekezwa kiutalii kama vile Uluguru, Udzungwa,etc. Tuna maziwa madogo madogo kama vile Eyasi, Ikimba, na mengineyo, tuna visiwa vidogovidogo. Tuna beach kibao ktk ukanda wa bahari ya pwani hazijaendelezwa, nenda kimbiji DSM huko utaziona. Vyote hivyo vina potential ya kuingiza pato la Taifa.
6. Serikali inaweza kupata pesa nyingi kwa kubana matumizi. Ukubwa wa serikali upungue, Baraza la mawaziri na manaibu wao ni wengi sana, ni msigo kwa Taifa. Magari kama vile V8 siyo afya kwa matumizi ya pesa za mlipa kodi
7. Serikali irahisishe international transactions. Nashangaa mpaka sasa watanzania hawawezi kutumia PAYPAL. Pesa nyingi sana ya kigeni inashindwa kuja nchini kwa sababu watu wanakosa kupata gatway ya malipo yao yatokayo nje wakifanya huduma hasa za ubunifu mitandaoni.
8. Serikali iondoe urasimu wa vyama vya ushirika na itoe uhuru wakulima hasa wa mazao ya biashara walime wawezavyo, na watafute soko wawezavyo, Serikali isubiri kodi. Siyo kuwapangia wakulima bei ya kuuza mazao yao na kuwalipa miezi kibao ijayo!