Kuna tofauti baina ya mjuzi na mweledi?Nimeona katika jukwaa la lugha kuna “English learning thread” yaani uzi unaohusiana na kujifunza lugha ya English.
Nahisi itakuwa vyema wahusika wakaanzisha uzi mwengine wa kujifunza lugha ya Kiswahili kwa sababu humu JF kuna watu wengi lugha ya Kiswahili inawapiga chenga kwani tunaona maandishi yao.
Si kila mwenye kuzungumza Kiswahili huwa Mswahili. Lugha ya Kiswahili ina wenyewe.
Wote wana sifa ya kujua jambo, ila mweledi anazingatia maadili ya ujuzi husika.Kuna tofauti baina ya mjuzi na mweledi?